Na Baraka Mbolembole
Timu ya Taifa ya Kenya ' Harambee Stars', leo itakata ' utepe' wa
michuano ya Mataifa ya ukanda wa CECAFA, kwa kucheza na timu ya Taifa ya Ethiopia. Wenyeji hao wa michuano ya sasa na makamu bingwa wa taji hilo, wanapewa nafasi kubwa ya kuvuka kundi A, mbele ya Ethiopia,
Zanzibar, na Sudan Kusini.
Mabingwa watetezi, Uganda wao wapo kundi C, pamoja na Rwanda, Sudan, na Eritrea katika kundi linalotarajiwa kuwa gumu zaidi katika michuano hiyo. Moi Kasarani na Nyayo Stadium, ni viwanja viwili vilivyopo
katika jiji la Nairobi, Kisumu Stadium, Mombasa, na Machakos ni idadi
ya viwanja vitano ambavyo vitazipokea timu 12. Mapema leo mchana wawakilishi wengine wa Tanzania, timu ya Zanzibar Heroes itacheza na Sudan Kusini katika mchezop wa kwanza kabisa mwaka huu.
KILIMANJARO STARS vs ZAMBIATimu
ya Taifa ya Tanzania Bara itaanza kibarua chake cha kwanza siku ya
kesho, Alhamis kwa kucheza na timu ' alikwa' ya Zambia katika mchezop
unaosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa soka. Zambia, mabingwa wa michuano
ya Mataifa ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika, COSAFA, iliifunga Kilimanjaro
Stars katika mchezo wa mwisho kukutana katika michuano hii,
walipoalikwa kwa michuano iliyofanyika, Dar es Salaam, 2010.
Mbele ya Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Stars ilipoteza kwa kulala bao 1-0 siku ya ufunguzi.
Disemba mwaka uliopita, Taifa Stars iliifunga timu ya Zambia kwa bao 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki huku ' Chipolopolo' wakiwa na nyota wao waliotwaa taji la mataifa ya Afrika, februari, 2012.

STARS, MATUMAINI YOTE KWA NGASSAMoja
kati ya silaha za hatari katika michuano hiyo ni kiungo mshambuliaji,
Mrisho Ngassa.
Ni mchezaji ambaye huvuta hisia kubwa za mashabiki hasa
timu yake inapokuwa nje ya Tanzania, kasi, ujanja, unyumbulifu, na
kucheza kwa kuhaha sehemu kubwa ya uwanja ni sifa ambazo zinampa nafasi
ya kipekee kutamba katika michuano hii.
Wakati, kocha wa Stars itambidi asubiri hadi mapema mwezi ujao kupata huduma za washambuliaji wake wawili, kati ya watatu katika safu ya mashambulizi, Mbwana Samatta na Tomas Ulimwengu, ambao watakuwa na mchezo wa marejeano wa fainali ya kombe la shirikisho Afrika, wikiendi hii wakiiwakilisha klabu yao ya TP Mazembe, Kim Poulsen atamtegemea mfungaji huyo bora wa michuano iliyopita nchini Uganda.
Elius Maguli, Juma Luizio, Joseph Kimwaga, na Amri Kiemba wawili kati yao wanataraji kuanza sambamba na Ngassa katika safu ya mashambulizi. Itakuwa ni nafasi nzuri kwao na pengine kijana Said Dilunga anaweza kufanya vizuri zaidi yao kama atapewa nafasi ya kutosha.
Katika nafasi ya kiungo, KIM, bado anao wachezaji ambao wana uwezo na uzoefu wa kutosha, SAlum Abubakary atakuwa akicheza michuano yake ya pili, sambamba na Frank Domayo na wawili hao waliweza kucheza vizuri japo waliambulia nafasi ya nee baada ya kufungwa na Zanzibar katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.

Kwa upande wa uzoefu itakuwa ni pigo kubwa
kwa Stars kama wachezaji hao vijana watashindwa kuendena na michuano kwa
kigezo cha uzoefu wao mdogo. Ni vijanma ambao wameshikilia namba katika
vilabu vyao vya Azam FC, na Yanga kwa zaidi ya miezi 14 sasa, na
wamekuwa chaguo la kwanza katika michezo zaidi ya 15 ya Kilimanjaro
Stars, na Taifa STars katika kipindi cha mwaka mmoja sasa
Wanatakiwa kujiamini zaidi na kuongeza umakini katika mchezo dhidi ya Zambia, timu ambao husifika kwa kasi yao mchezoni na mchezo wa pasi za haraka haraka zile fupifupi, Kwa, Salum sina shaka ataweza kuwazima kama ilivyo kawaida yake, ni mtaalamu wa pasi fupi na ndefu, ni nadra kupoteza au kupiga pasi ' fyongo' uwanjani, wakati Domayo akisifika kwa utulivu wake, bado viongo hao wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kushindwa kutengeneza nafasi za mwisho japo muda mwingine huoneka kumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa.
Wakati, Samatta na Ulimwengu tukisubiri huduma zao silaha yetu kubwa sasa ni Ngassa, ni vipi tunaweza kumchezesha na akaisadia timu, mbio zake, akili yake na uwezo wake alionao wa kutambua afanye nini atapokuwa amefika katika lango la adui, Domayo anaweza kupiga pasi ndefu zilizotimilifu itakuwa vyema kumtumia huyu kupiga pasi za haraka kwa Ngassa. Ni wazi Zambia watamili mpira mpira hiyo ni kutokana na namna tunavyoshindwa kuwa mashindanoni. Kwa nini nasema hivyo? Wakati mwingine ni lazima tuwe wazi wachezaji wetu hutuangusha hasa pale tunapokuwa tunaweka imani kubwa juu yao.
Kufungwa michezo mitatu, kati ya sita katika michuano iliyopita ni sawa na kutoa udhibitisho huo, wakati tulipofungwa mchezo wa kwanza na Burundi, ilitukumbusha kupandisha kiwango chetu cha uchezaji, hiyo ilitusaidia hadi kuwa na wafungaji bora wawili siku ya mwisho wa michuano. Tulicheza vizuri katika michezo miwili tu iliyofuata, lakini kipigo kutoka kwa Uganda kilikuwa ni ' kizito sana' katika vichwa vya mashabiki wa soka nchini.
Tulifungwa kidhaifu sana katika mchezo wa nusu fainali huku
Watanzania wakiamini kuwa ilikuwa nafasi yetu kuvunja utawala wa zaidi
ya miaka kumi wa Uganda kutofungwa nyumbani.
Uzoefu wa wachezaji kama Kelvin Yondan, Athumani Idd ' Chuji' , Kiemba, Ngassa, Erasto Nyoni, Ivo Mapunda, usiishie katika uwakilishi wa uwanjani tu, wanatakiwa kuwakumbusha wachezaji vijana kama kina Ramadhani Singano, Domayo, Dilunga, Kimwaga na wengine umuhimu wa kuona fahari kushinda mataji wakiwa katika jezi ya taifa.
Wakati tulipopata
taji la mwisho mwaka 2010 kuna vijana ambao walitoka mitaani na kupata
nafasi ya kukutana na watawala wa juu wa nchini. Ni fahari kuichezea
timu yako ya Taifa.
Ila mafanikio ndiyo kipimo sahihi cha ubora wa jambo
lolote. HIvyo wachezaji wanatakiwa kufahamu kuwa tangu kizazi na kizazi
wapo wachezaji ambao wamekuwa wakiiwakilisha nchi, ila wale
waliofanikiwa kushinda chochote ndiyo waliopata nafasi ya kufika
bungeni, ikulu na sehemu nyingine ambazo si rahisi kufika.
KUJIAMINI KUPITA KIASIJapo
umakini limekuwa tatizo kubwa kwa Stars, kujiamini kupitiliza imekuwa
ni sumu ambayo imekuwa ikituangamiza sisi wenyewe.
Watazame, Salum,
Domayo na safu ya ulinzi. JInsi wanavyokuwa wanacheza wakati tukimiliki
mpira imekuwa kama hawajui umuhimu wa kutengeza nafasi za kufunga mabao.
Hii ni michuano ya mtoano. Nafasi moja, bao moja, kufungwa inamaanisha
kuwa mchezo ujao utakuwa ni mgumu kuliko kama mngeshinda, na nafasi
inakuwa ndogo ya kusawazisha mambo.
Safu ya ulinzi, Nyoni, anatakiwa kupevuka kiuchezaji sasa na kuacha na soka la ' kipima joto', huwa hatabiriki , ingawa akiwa katika siku yake nzuri utapenda kuona anavyokuwa akiisaidia timu katika mashambulizi na kuzuia, ila akiwa hovyo utatamani apasi, akisumbuliwa mara mbili au tatu hupoteza kujiamini na umakini wake unakuwa chini zaidi. Kwa kifupi safu za ulinzi wa pembeni zikiwa imara na kufanya kazi ipasavyo hufanya ulinzi wote kuimarika, ila wakiwa katika kiwango cha kupoteza mipira hovyo na kushindwa kujiamini katika maamuzi yao hupelekea kuvuruga mambo na wakati walinzi wa kati wakishirikiana na viungo kujaribu kuweka mambo sawa mara nyingi tunajikuta tukipotea kabisa uwanjani. Wachezaji wa ulinzi watakiwa kucheza soka lililokamilika kwa wakati huu wakiwa na michezo mingi katika historia yao.
" Kama utacheza vizuri na kushinda hilo ni bora, ila kama hautocheza vizuri kwa namna yoyote ile, hakikisha ushanda kwa namna yoyote" aliwahi kusema, Luis Aragones, kocha wa kwanza kuipa Hispania taji baada za kupita miaka zaidi ya 40.

BURUNDI, UGANDA, ETHIOPIAStars
itacheza tena na Burundi katika kundi la B, na matokeo yao dhidi ya '
Risasi za Shaba' hapo kesho yanaweza kuufanya mchezo dhidi ya makamu
bingwa hao wa mwaka 2004 kuwa mgumu zaidi na kuamua hatma ya kundi.
Mwaka jana bao lililofungwa na Suleimani Ndikumana lilizamisha Stars
nchini Uganda katika mchezo wa hatua ya makundi. Burundi, sambamba na
Uganda, na Ethiopia wanaitumia michuano hii ili kujiweka sawa na
michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani,
CHAN 2014, nchini Afrika ya Kusini, mapema mwaka ujao.
TAKWIMU
Hizi ni takwimu za kila nchi katika michuano hiyo tangu kuanzishwa.
Namba ni nafasi ambayo timu huonesha ilimazima katika nafasi gani
1'
Huonesha ni nafasi ya kwanza, Namba mbili huwakilisha nafasi ya pili,
Namba tatu kwa nafasi ya tatu kama ilivyo kwa namba nne kwa nafasi ya
nne.
Burundi
1 –
2 2004
3 –
4 1999, 2007, 2008
Ivory Coast
1 –
2 2010[b][i]
3 –
4 –
Eritrea
1 –
2 –
3 –
4 1994
Ethiopia
1 1987, 2001, 2004, 2005
2 –
3 2000
4 1995, 2010
Kenya
1 1975, 1981, 1982, 1983, 2002
2 1979, 1985, 1991, 1999, 2001, 2008, 2012
3 1978, 1988, 1989, 1994, 1995, 2003
4 1977, 1984, 1996, 2004
Malawi[i]
1 1978, 1979, 1988
2 1975, 1984, 1989
3 1977, 1980, 1985
4 1983, 1992
Rwanda
1 1999[b]
2 2003, 2005, 2007, 2009, 2011
3 1999, 2001, 2002, 2006
4 2000, 2001[b]
Sudan
1 1980, 2006, 2007
2 1990, 1996[b]
3 1996, 2004, 2011
4 1991, 2003
Tanzania
1 1974, 1994, 2010
2 1973, 1980, 1981, 1992[b], 2002
3 1979, 1990, 2008
4 2009, 2011, 2012
Uganda
1 1973, 1976, 1977, 1989, 1990, 1992, 1996, 2000, 2003, 2008, 2009, 2011, 2012
2 1974, 1982, 1994, 1995[b], 2000
3 1983, 1984, 1987, 1991, 2007, 2010
4 1978, 1981, 1985, 2002, 2005, 2006
Zambia[i]
1 1984, 1991
2 1976, 1977, 1978, 1988, 2006
3 1981, 1992
4 1980, 1989
Zanzibar
1 1995
2 –
3 2005, 2009, 2012
4 1979, 1982, 1987, 1990
Zimbabwe[i]
1 1985
2 1983, 1987
3 1982
4 1988
By number of titles won and editions participated in
Team 1ST 2ND 3RD 4TH Pld Pldlst
Uganda 13 5 6 6 35 2012
Kenya 5 7 6 4 34 2012
Ethiopia 4 – 1 2 17 2012
Tanzania 3 5 3 3 33 2012
Malawi 3 3 3 2 21 2012
Sudan 3 2 3 2 19 2012
Zambia 2 5 2 2 20 2010
Zimbabwe 1 2 1 1 16 2012
Zanzibar 1 – 3 4 32 2012
Rwanda B 1 – – – 2 2001
Rwanda – 5 4 2 16 2012
Burundi – 1 – 3 13 2012
Côte d'Ivoire B – 1 – – 1 2010
Eritrea – – – 1 10 2012
Djibouti – – – – 10 2011
Kenya B – – – – 2 1994
Seychelles – – – – 2 1994
Somalia – – – – 23 2012
South Sudan – – – – 1 2012
Sudan B – – – – 1 1996
Tanzania B – – – – 1 1992
Uganda B – – – – 2 2000
Zimbabwe U23 – – – – 1 2
No comments:
Post a Comment