Monday, December 01, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA ASSAD KUWA CAG MPYA


Profesa Mussa Juma Assad 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz 

BOKO HARAM WAVAMIA MIJI MIWILI NIGERIA

Nia kuu ya Boko Haram ni kuwa na dola ya kiisilamu inayofuata sheria za kiisilamu.
 
Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamefanya mashambulizi katika miji miwili eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
La kwanza lilikuwa la kujitoa mhanga pamoja na shambulizi lengine katika kituo cha polisi cha Damaturu.
Wenyeji wa mji wa Maiduguri walielezea kusikia milipuko miwili kwenye soko moja.
Mashambulizi mengine ya kujitoa mhanga eneo hilo wiki iliyopita yaliwaua zaidi ya watu 70.
Mapema leo Jumatatu watu wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliteketeza kituo cha polisi katika mji wa Damataru kilicho umbali wa kilomita 100 Magharibi mwa mji wa Maiduguri.
Inaarifiwa watu 5 wameuawa katika mashambulizi hayo ya mabomu yaliyotokea katika soko lililokuwa na watu wengi.
Mjini Damaturu , milipuko na milio ya risasi ilisikika huku wanamgambo hao walipokuwa wanashambulia mjini huo.
Boko Haram imeahidi kubuni dola ya kiisilamu katika maeneo ambayo kundi hilo linadhibiti.
Milipuko hio ilitokea Jumatatu katika soko la Maiduguri , mji mkuu wa jimbo la Borno ambayo ilisababishwa na wasichana wawili waliojilipua.
Takriban watu 32 walijeruhiwa katika milipuko hio. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ICC YAKATAA OMBI LA MUASI LUBANGA

Mahakama ya ICC imetupilia mbali ombi la Lubanga kupunguziwa kifungo jela.
 
Mahakama ya kimataifa ya ICC mjini Hague, imetupilia mbali ombi la rufaa lililowasilishwa na muasi wa zamani nchini DRC Thomas Lubanga dhidi ya hukumu aliyopewa kwa makosa ya kuwatumia watoto kama wanajeshi.
Viongozi wa mashtaka walisema wavulana wadogo wenye umri wa miaka 10 walitekwa nyara na kusajiliwa kama wanajeshi DRC katika vita hivyo vilivyoanza mwaka 1999.
Wasichana nao walitumiwa kama watumwa wa ngono.
Mnamo mwaka 2012, Lubanga alikuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama hio.
Aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji la (UPC), ambalo lilikuwa la kabila la Hema ambalo lilihusika katika vita eneo la Ituri Mashariki mwa DRC.
Mahakama ilimpata na hatia kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi na kuwatuma kwenda kumpigania. Alihukumiwa kifungo cha miaka 14.
Kundi la UPC, lilikuwa moja ya makundi sita ya wapiganaji waliopigana kudhibiti eneo lenye utajiri wa madini la Ituri hadi mwaka 2003.
Mgogoro ulianza kama mvutano wa kupigania mali asili, ingawa baadaye ilipanda daraja na kuwa vita vilivyohusisha jeshi la Uganda.
Kadhalika mgogoro huo uligeuka na kuwa vita kati ya jamii za Hema na Lendu ambapo takriban watu 50,000 waliachwa bila makao. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...