Wednesday, November 13, 2013

SNURA WA MAJANGA ALETA SHIDA, KWELI HII NI BALAA DUNIANI....!!!


 Ilikuwa kwenye show ya kichwaji cha GRAND MALT maeneo ya karumeshida ilianza pale mkali wa viuno mwanadada snura alivyopanda jukwaaani hali ilikuwa si shwali kabisa pale wauza mitumba waliaamua kupiga shangwe za hatari na kutaka mpaka kumshika snura kwa balaa alilolifanya. show ilivyoisha alitumia lisali moja na nusu kutoka kaatika uwanja huo kila mtu alitamani kumshika kila mtu alitaka kupiga nae picha. angalia video hapo chini hali ilivyokuwa.

MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY

Stori:  Jelard Lucas
HILI ndiyo Risasi bwana! Sikia, kama ulikuwa hujui ni kwamba msanii mkongwe katika filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kueleza mengi ikiwemo kutoa mimba ya mpenzi wake wa siku nyingi, Vincent Kigosi, tulia hapohapo.

Mbali na uhusiano wao huo uliokuwa ukifanywa siri, Mainda ameeleza kwa machungu jinsi Ray alivyomtesa kwa kumchanganya na wasanii wenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu.

Risasi Mchanganyiko lilipata wasaa wa kufanya naye mahojiano ‘exculusive’ kwa saa moja na dakika tano, wikiendi iliyopita, makao makuu ya gazeti hili, Mwenge – Bamaga, jijini Dar.

Hata hivyo, alisema uhusiano wao kwa sasa umevunjika rasmi huku akibainisha jinsi alivyonyooshewa vidole na watu wakiamini kwamba aliambukizwa Ukimwi na aliyekuwa mpenzi wake kabla ya Ray, marehemu Said Maulid Banda  ‘Maxi’.
Soma mwenyewe mahojiano yalivyokuwa mstari kwa mstari, neno kwa neno:

Risasi: Baada ya kifo cha Maxi, Ray alijitokeza na kukutongoza au siyo?
Mainda: Hapana, nakumbuka ilikuwa Siku ya Valentine’s Day mwaka 2004...sikumbuki kama tulitongozana ama vipi lakini ilitokea tukajikuta kwenye uhusiano.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KIFO CHA DK MVUNGI KUTOKA CHADEMA

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salaam za rambirambi ya kifo cha Dkt. Edmund Sengondo Mvungi, akitoa pole kwa familia, uongozi na wanachama wa NCCR-Mageuzi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya na wananchi wote walioguswa na msiba huo. Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wa chama hicho, Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa amepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa za kifo cha Dkt. Mvungi, akimwelezea kuwa alikuwa mwanasiasa mwenye msimamo ambaye hakuwahi kutetereka kusimama na chama chake tangu alipojiunga nacho na kuanza kushiriki siasa za mageuzi nchini. “Kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wetu nchi nzima, napenda kutoa salaam za pole sana kwa familia ya marehemu, mjane na watoto. Natoa pole kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wanachama wa chama hicho, pia tunatoa pole kwa Jaji Mstaafu Joseph Warioba na makamishna wote wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwakifo cha Dkt. Mvungi. Tunaomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu sana wakati huu wa majaribu na majonzi makubwa. “Dkt. Mvungi alikuwa mwanasiasa mwenye misimamo ambaye hakuwahi kukihama chama chake tangu alipoanza siasa za mageuzi nchini. Ni kati ya wasomi wachache waliokuwa na ujasiri na kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani tangu mapema. "Mvungi pia alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa kupigania nchi yetu iwe na Katiba Mpya, ili hatimaye siasa zetu, hususan demokrasia ya vyama vingi nchini iendeshwe kwa misingi iliyo imara,” amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza; “Mwenyezi Mungu alimjalia marehemu akaweza kushiriki kutimiza ndoto hiyo baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Mpya, kazi ambayo ameifanya hadi siku alipokutwa na tukio lililosababisha mauti yake.” Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, amesisitiza kuwa kwa namna ambavyo Dkt. Mvungi alikuwa mstari wa mbele katika suala hilo, Tume ya Katiba Mpya inao wajibu wa kuthamini mchango wake katika hatua iliyofikia sasa ya mchakato huo nyeti hadi utakapofika mwisho. “Wakati tukimwombea marehemu kwa Mungu, alazwe mahali pema peponi, ni matumaini yetu kuwa serikali kupitia vyombo vyake itahakikisha kuwa wale wote waliohusika katika tukio la lililosababisha kukatisha uhai wa Dkt. Mvungi wanapatikana na kuchukuliwa hatua zote zinazostahili kisheria,” amesema Mwenyekiti Mbowe.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 13, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.

HABARI ZAIDI JUU YA KIFO CHA DR. SENGONDO MVUNGI

Mvungi_01_2d4e9.jpg
Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania imepata pigo baada ya mmoja wa wajumbe wake Dr. Sengondo Mvungi kufariki dunia nchini Afrika Kusini, ambako alikuwa akitibiwa.
Dr. Mvungi, alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kuvamiwa na watu wanaoaminika kuwa majambazi nyumbani kwake mjini Dar, es Salaam, wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid Dkt. Mvungi alifariki majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.
"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo Jumanne, Novemba 12, 2013 saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bwana Rashid katika taarifa yake fupi.
Amesema taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini Tanzania kwa mazishi zinaendelea.
Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) alipokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake.
Dkt. Mvungi pamoja na kuwa ni mwanasheria aliyebobea katika fani ya Katiba, pia ni mwanasiasa ambaye aliwahi kugombea urais mwaka 2005 kupitia chama cha NCCR Mageuzi.

MWANAKANDANDA AADHIBIWA NCHINI MISRI KISA KUSHANGILIA ALAMA YA VIDOLE

131111211449_ahmed_abdul_zaher_rabaa_464x261_afp_nocredit_e73c9.jpg
Ahmed Abdul Zaher amejitetea akisema hakunuia kuzua hisia za kisiasa
Mchezaji soka mmoja katika moja ya vilabu maarufu nchini Misri ametupwa nje ya mechi za klabu hiyo baada ya kuonekana kumuunga mkono rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi.
Klabu ya Al Ahly, imesema kuwa Ahmed Abdul Zaher , hatashiriki mchuano wa FIFA wa klabu bingwa duniani baada ya kupiga saluti ya vidole vinne mnamo siku ya Jumapili.
Mchezaji huyo alikuwa anasherehekea bao lake la mchuano wa mabingwa wa Afrika ambapo Al Ahly ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Orlando Pirates wa Afrika Kusini.
Ishara hio imekuwa ikitumika kama ishara ya kumuunga mkono bwana Morsi.
Ishara hiyo pia ilitokana na maandamano ya wafuasi wa Morsi waliotawanywa na maafisa wa usalama mnamo mwezi Agosti baada ya kukesha katika eneo walilosema alikuwa amezuiliwa Morsi.
Rais Morsi alikuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia, na sasa anakabiliwa na kesi ya kuchochea mauaji ya waandamanaji wakati wa ghasia zilizotokea mjini Cairo mwaka jana.
Yeye mwenyewe aling'olewa kutoka uongozini mwezi Julai.
Abdul Zaher alisherehekea kwa ishara ya vidole vinne baada ya kuingiza bao la Al Ahly la pili ambapo waliibuka washindi dhidi ya Orlando Pirates.
"ndio nilitoa ishara hiyo ya Rabaa," alinukuliwa akisema kwenye mtandao wa FilGoal.
"lakini sikunuia kuzua hisia za kisiasa kwa mtu yeyote, nilichonuia ni kumkumbuka mtu yeyote aliyefariki, awe raia wa kawaida au hata polisi.''
Mnamo siku ya Jumatatu maafisa wa klabu ya Al Ahly, walisema kuwa Ahmed Abdul Zaher hatashirikishwa kwenye mechi itakayochezwa nchini Morocco.

JK AKATAA ZAWADI YA PANDE LA DHAHABU

jk_taifa_1b3a9.jpg
Rais Jakaya Kikwete jana aligoma kupokea zawadi ya dhahabu kutoka Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya mkoani Geita.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana ilisema viongozi wa kampuni hiyo walitaka kumkabidhi Rais Kikwete gramu 227 za dhahabu safi wakati alipotembelea mgodi huo.
Rais Kikwete badala yake aliwaelekeza waiuze dhahabu na fedha zitakazopatikana zitumike kuwasaidia watoto yatima.
Alikabidhiwa zawadi hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma ambao ni makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang'hwale, Geita.
Gramu hizo 227 zina thamani ya Sh16 milioni kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.
Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete aliuliza: "Sasa nifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima."
Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete aliupongeza uongozi wa mgodi huo akisema umeongeza thamani ya dhahabu na maisha ya wananchi katika eneo hilo... "Mmefanya vizuri na mgodi huu, ni mradi wa maana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifu huu unastahili pongezi," alisema Rais Kikwete.

WINGI WA SAFARI ZA MESSI WACHANGIA MAUMIVU YA MARA KWA MARA.

Ndani ya siku 64 Lionel Messi ameizunguka dunia kwa kusafiri jumla ya 122,333 KM, alipozitembelea nchi na miji mbali mbali kwa ajili ya shughuli za kibalozi na kutengeneza matangazo,miongoni mwa nchi na miji aliyotembelea ni Senegal, Argentina , Ecuador, Peru, Colombia, Guatemala, Los Angeles, Las Vegas, Chicago, Norway, Germany, Poland, Barcelona, Milan, Israel, Palestine, Thailand and Malaysia.

KAMPENI YA NANI MTANI JEMBE SASA YAHAMIA KANDA YA KASKAZINI. WATALII WAKATA MAUNO BALAA....!!!



Wakazi wa eneo la Maji ya Chai, Arusha wakiangalia burudani iliyokuwa inatolewa na timu ya kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe’ inayohusisha mashabiki Simba na Yanga,  ili kuzipigia kura timu zao na kushinda kitita kingi kati ya Tsh.100 milioni zilizotelewa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ndio wadhamini wa timu hizo na timu ya Taifa. 
Timu hiyo ipo kanda ya Kaskazini na Mashariki inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida na Tanga.






Watalii kutoka nchi mbalimbali wakicheza pamoja na washereheshaji wa kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe’ inayohusisha mashabiki Simba na Yanga,  ili kuzipigia kura timu zao na kushinda kitita kingi kati ya Tsh.100 milioni zilizotelewa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ndio wadhamini wa timu hizo na timu ya Taifa. 
Timu hiyo ipo kanda ya Kaskazini na Mashariki inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida na Tanga. Watalii hao walikuwa wakitembelea maeneo mbalimbali mkoani Arusha

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...