Wednesday, January 25, 2017

ECOWAS WABAINI KEMIKALI YA SUMU IKULU YA GAMBIA

Rais mstaafu wa Gambia Yahya Jammeh

Askari wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) wamegundua kemikali ya sumu kali iliyokuwa imetegwa kwenye vyumba vya Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ecowas kupitia gazeti la Freedom la Gambia, kemikali hiyo ilitegwa kwa lengo la kuua mtu yeyote atakayeingia ndani ya Ikulu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi mpya wa Gambia, Adama Barrow anatakiwa kuendelea kukaa Senegal kwa usalama wake huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

CUF WAMGEUKIA JENERALI MWAMNYANGE

Kikao cha kutathmini uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani  cha  Chama cha  Wananchi (CUF), kimekusudia kumwandikia barua ya malalamiko Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange wakidai wanajeshi walishiriki kuleta hofu.

Hata hivyo, jeshi hilo limekana madai ya CUF likisema ni uzushi.

Madai hayo yalitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alipozungumza kwa simu na mwandishi wetu kuhusu uamuzi wa kikao hicho kilichofanyika jana Unguja chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na kuhudhuriwa na wajumbe 14.

Alidai kikao hicho kilichojadili mwenendo mzima wa uchaguzi kuanzia kampeni, kilifikia uamuzi wa kuandika barua ya malalamiko kwa Jenerali Mwamunyange wakidai wanajeshi walionekana wakizunguka mitaani katika jimbo, siku ya kuamkia uchaguzi na siku ya kupigakura.

FUMANIZI FEKI ZATIKISA MOSHI NA ARUSHA

(picha na maktaba) 

Utapeli wa aina yake unazidi kutikisa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha baada ya kuibuka matukio ya kupangwa ya kufumania watu wenye heshima katika jamii kwa lengo la kujipatia fedha.

Siku za karibuni kumekuwa na mlolongo wa matukio hayo, yakiwalenga viongozi wa kiroho, wanandoa na vigogo wenye nyadhifa serikalini.

Uchunguzi ulibaini utekelezaji wa matukio hayo huambatana na vitisho kwa walengwa, ikiwamo kuwapiga picha na baadaye kutakiwa kutoa fedha kati ya Sh milioni 5 na Sh milioni 15 ili tukio hilo lisichapishwe kwenye vyombo vya habari.

Wake au waume za watu, viongozi wa dini na watendaji serikalini ndiyo walengwa wakuu wa matukio hayo, kwa kuwa ndiyo wenye hofu ya kuvunjiwa heshima kwenye jamii.

Chanzo: Mwananchi.

IVORY COAST YATUPWA NJE YA AFCON

Wachezaji wa Morocco wakishangilia.

Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la mataifa ya afrika tembo wa Africa Ivory Coast, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu baada ya kuchapwa kwa bao 1-0 na Simba wa Atlas Moroco

Goli pekee liliowaondoa miamba hao wa soka wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo.

Nayo timu ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo ilitambia Togo kwa kuichapa kwa mabao 3-1 na hivyo kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara kwa kundi C kwa alama 7 huku Moroco wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Moroco na Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo wanafuzu katika kundi hilo la huku Ivory Coast na Togo zikitupwa nje ya michuano hiyo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...