Wastani wa umri
wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kutoka miaka 50 kwa sensa
iliyofanywa mwaka 1988 hadi kufikia miaka 61 kwa sensa ya mwaka 2012.
Akiwasilisha taarifa za msingi za kidemografia,
kijamii na kiuchumi kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini hapa
jana, mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina
Chuwa alisema wanawake wanaishi umri mrefu zaidi kuliko wanaume.
“Matokeo haya yameendelea kuonyesha wastani wa
umri wa kuishi kwa wanawake ni miaka 63 ambao ni mkubwa zaidi
ukilinganisha na wanaume ambao ni miaka 60. Tunaamini ongezeko hilo
limetokana na kukua kwa uchumi na kupungua kwa umaskini wa kipato.”
Akizungumzia kuhusu matokeo ya awali ya uzazi kwa
sensa ya mwaka 2012, alisema inaashiria kupungua kwa kiwango cha uzazi
kutoka wastani wa watoto 6.5 mwaka 1988 hadi kufikia watoto 5.2.
“Hii inaweza kuwa imesababishwa kuongezeka kwa
umri wa kuolewa katika umri wa kuanzia miaka 22 wakati wanaume
wamebainika kuwa huoa kuanzia miaka 24 na kuendelea,” alisema.
Alisisitiza kuwa inawezekana matumizi ya njia za
kisasa za uzazi wa mpango na kuongezeka kwa kiwango cha elimu kwa
wanawake ni sababu zinazowafanya waishi zaidi. Akizindua taarifa hiyo,
Rais Jakaya Kikwete aliwapongezawalioshiriki kukusanya taarifa hizo na
kuzichanganua, akieleza kwamba ni miongoni mwa shughuli ngumu kwa kuwa
kuna udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Taarifa hizi zimechambuliwa vyema na zitasaidia
kupanga masuala ya maendeleo. Idadi yetu inazidi kuongezeka pia. Mwaka
2012 tulikuwa milioni 44, pengine hadi mwaka 2016 tutakuwa milioni 48,”
alisema.
Na Mwananchi
Na Mwananchi