Sunday, November 02, 2014

MCHUNGAJI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA ZA BIL. 2 ZA KITANZNIA...!!!

dawaaa
Jeshi la Polisi kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata kilo 40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya shilingi bilioni 2.
Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.
Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia Gazeti la MTANZANIA kuwa  kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.
“Ni kweli tukio la aina hiyo lipo  lakini watu kama hawa siwezi kusema moja kwa moja ni Mchungaji  ndio muhusika hadi nipate vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara hii,”Alisema Nzowa.
Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya kuweka hadharani ukweli wa mambo. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ANGALIA PICHA ZA MAPOKEZI YA MWILI WA ALIYEKUWA RAIS WA ZAMBIA, MICHAEL SATA

Mwili wa Rais wa Zambia, Michael Sata umewasili Zambia tayari kwa mazishi ambayo yamepangwa kufanyika November 11.

Mwili wa rais huyo umewasili uwanja wa ndege wa Kenneth Kaunda International Airport na kupelekwa Mulungushi International Conference Centre kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine zilizopangwa na Serikali ya nchi hiyo kufanyika kabla ya mazishi.
Hizi ni picha 10 zikionyesha namna mapokezi yalivyokuwa katika jiji la Lusaka siku ya jana Novemba 1.
Sata4
Sata5 
Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 02, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KAMBI YA JESHI YAVAMIWA...!!!

wanajeshi katika kambi
Wanajeshi katika kambi ya jeshi ya Nyali iliopo mjini Mombasa pwani ya Kenya wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 6 baada ya genge la wahalifu kuvamia kituo hicho cha jeshi mapema leo.
Inadaiwa kuwa kundi la watu 15 lilijaribu kuvamia kambi hiyo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ya jumapili.
Wanajeshi waliokuwa katika zamu waliweza kulidhibiti kundi hilo ambapo watu watano waliuawa huku askari mmoja akiweza kujeruhiwa kwa kukatwa na mapanga na wavamizi hao.
Kufikia sasa maafisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha shambulizi jilo.
Hatahivyo wengi wanashuku watu hao huenda ni wanachama wa kundi la Mombasa Republican Council MRC.
Lakini msemaji wa kundi hilo Randu Nzai amekanusha habari hizo akisema kuwa kundi hilo halikuhusika kamwe. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

WATU WA BENI WAANDAMANA

Ripoti zinasema kuwa maandamano yamefanywa katika mji wa Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, baada ya mauaji ya karibuni yaliyofanywa na wapiganaji.
Kituo cha redio cha huko kinasema kuwa waandamanaji wanaodai ulinzi zaidi, wameshambulia sanamu ya Rais Joseph Kabila saa chache baada ya kujulikana kuwa watu 7 zaidi waliuwawa Jumamosi usiku.
Inakisiwa kuwa watu kama 100 wameuwawa katika eneo la Beni katika mwezi uliopita.
Wanaoshukiwa kufanya hayo ni wapiganaji wa ADF - kundi la wapiganaji Waislamu kutoka Uganda ambao sasa wanapigana na jeshi la Congo na askari wa Umoja wa Mataifa.
Alipozuru mji wa Beni Ijumaa, Rais Kabila aliahidi ulinzi zaidi kwa raia na aliomba kuwa kikosi cha Umoja wa Mataifa huko kizidishwe. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...