Saturday, October 18, 2014

'MEYA TABORA AMILIKI BODA BODA 400'


Meya wa Manispaa ya Tabora, Gullam Hussein Dewji akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam jana, baada ya kutoka kwenye Baraza ka Maadili ya Viongozi, alikoitwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kujilimbikizia mali na matumizi mabaya ya madaraka. 


Dar es Salaam. Meya wa Manispaa ya Tabora, Gulam Hussein Dewji ameshushiwa tuhuma nzito za kuidanganya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushindwa kutangaza mali anazozimikiki zikiwamo pikipiki 422, licha ya kutakiwa kufanya hivyo kisheria.

Sheria Namba 5 ya mwaka 2001 ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inamtaka kila kiongozi kujaza fomu za kutangaza mali zake na madeni na kuziwasilisha kwenye Sekretarieti hiyo kila mwisho wa mwaka.

Meya huyo alisomewa mashtaka yake jana na Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Hamisi Msumi.

Mwanasheria huyo alisema kuwa meya huyo anatuhumiwa kutotamka baadhi ya mali anazozimiliki na kuzitaja mali hizo kuwa ni pikipiki 422, magari matatu, viwanja vitano na nyumba moja.

Cyriacus alisema kwamba meya huyo alishindwa kutangaza mali zake katika kipidi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2010 hadi 2013. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KAMPENI URAIS CCM: NOTI ZAMWAGWA DODOMA


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), wakiwa katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa White House mjini Dodoma juzi na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete. 

Baadhi ya makada wa wa CCM wanaotajwa kuwania urais kupitia chama hicho wanadaiwa kugeuza mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), kuwa sehemu ya kampeni kwa wajumbe wa mkutano huo wakidaiwa kumwaga fedha usiku kucha.

Gazeti hili lilishuhudia kampeni hizo zikifanywa na wapambe wa wagombea hao nje ya Ukumbi wa Nec uliopo nje ya jengo la White House mjini Dodoma na baadhi ya watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo.

Wapambe hao kwa siku mbili za vikao vya Nec vilivyofanyika mjini hapa kuanzia juzi walionekana wakifika mapema, kusalimia, kujitenga katika makundi madogomadogo na wajumbe wa Nec tofauti na vikao vingine vilivyotangulia.

Harakati hizo hazikuishia katika viwanja hivyo, bali hata nje ambapo mmoja wa makada anayetajwa kuwania nafasi hiyo kutoka Kanda ya Ziwa ameonekana kukutana na makatibu wa CCM katika moja ya hoteli mjini hapa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DK. SHEIN APATA MPINZANI URAIS ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein  
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein, amepata mpinzani iwapo ataamua tena kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao mwakani, baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Tadea, Juma Ali Khatib (50), kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo visiwani humu.

Mgombea huyo ni watatu kujitokeza hadharani na kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo, baada ya katibu mkuu wa CUF, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kutangaza nia hiyo akifuatiwa na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed aliyetangaza pia nia hiyo.

Hamad Rashid alitangaza nia na kusema kuwa atawania nafasi hiyo kupitia CUF, mgombea binafsi au kwa tiketi Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

Ikiwa Maalim Seif atawania tena nafasi hiyo, itakuwa ni mara ya tano tangu mwaka 1995, ulipoanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 18, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RIPOTI MAALUM: WAFUNGWA WAENDESHA UHALIFU GEREZANI


Pingu za wahalifu

Wakati Serikali ikihaha kukabiliana na vitendo vya uhalifu, imebainika kuwapo kwa mtandao wa uhalifu ambao unawawezesha baadhi ya watu waliofungwa kuratibu matukio ya uhalifu wakiwa gerezani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Uchunguzi wa gazeti hili katika eneo hilo uliojumuisha Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kigoma, umebaini kuwa uhalifu huo unahusisha ujambazi, mauaji ya kukodiwa na ujangili wa wanyamapori na watuhumiwa wanatajwa kuwa ni baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa.

Kutokana na nguvu uliyonayo, mtandao huo umekuwa ukitekeleza vitendo vya uhalifu kwa kufanya mawasiliano na watu wao waliofungwa kifungoni kwa kutumia askari na watendaji wengine wa Serikali wasio waaminifu.

Kwa nyakati tofauti watendaji wakuu wa polisi na magereza katika mikoa hiyo, wamezungumzia hali hiyo na baadhi wakionyesha kukiri kwa kueleza; ‘uhalifu wowote lazima uwe na mtandao na kwamba mtu yeyote anaweza kuwa mhalifu.’ Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UN YATETEA JUHUDI ZA KUAANGAMIZA EBOLA

David Nabarro katikati
Mratibu wa shughuli za Umoja wa mataifa kuhusu ugonjwa wa ebola Davis Nabarro ametetea juhudi za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo magharibi mwa afrika.
Bwana Nabbaro alikuwa akijibu shutma kutoka kwa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF lililosema kuwa ahadi za misaada hazijakuwa na mafaniko yoyote katika vita dhidi ya ugonjwa wa ebola.
Ameiambia BBC kuwa mipango iko njiani ya kutoa vitanda 4000 kwa wagonjwa wa ebola ifikiapo mwezi ujao.
Matamshi yake yanajiri baada ya ripoti ya ndani ya shirika la afya duniani inayosema kuwa WHO imeshindwa kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM KUWAACHIA WANAFUNZI




Wanafunzi wa Chibok waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram

Serikali ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.
Mkuu wa jeshi la Nigeria Alex Badeh,aliyefichua makubaliano hayo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon anasema kuwa wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo.
Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.
Kulingana na afisaa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais wa Chad Idris Derby.
Alisema kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika mkutano mwingine utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.
Pia alieleza kwamba maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo na kwamba wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...