Thursday, July 18, 2013
WASTARA JUMA "NAHITAJI MUME NA SI MWANAUME WA KUPITA"
STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma amesema hana haraka ya kuolewa kwani anahitaji mume na si mwanaume wa kupita
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kwa sasa yupo huru kutoka na mtu yeyote ampendaye kutokana na sheria na dini inavyosema ila kwa sasa shughuli za kuigiza zimembana.
‘Nahitaji mume na si mwanaume wa kupita, awe mvumilivu, mchapakazi pia awe na hofu ya Mungu. Kwa sasa nafanya filamu zangu kama kumuenzi marehemu mume wangu,” alisema Wastara.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kwa sasa yupo huru kutoka na mtu yeyote ampendaye kutokana na sheria na dini inavyosema ila kwa sasa shughuli za kuigiza zimembana.
‘Nahitaji mume na si mwanaume wa kupita, awe mvumilivu, mchapakazi pia awe na hofu ya Mungu. Kwa sasa nafanya filamu zangu kama kumuenzi marehemu mume wangu,” alisema Wastara.
Na GPL
UJUE UKWELI WA DAWA ZA KULEVYA WALIZOKAMATWA NAZO MASOGANGE NA MWENZAKE, ADHABU YAO MIAKA 20 AU KIFUNGO CHA MAISHA
Mellis Edward kushoto na Agness Masogange kulia waliokamatwa na madawa ya kulevya nchini Afrika kusini
****
BAADA
ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii
anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes
Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba
dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo
hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.
Kupitia
taarifa rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa
walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini
Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza
ofisini kwake Dar es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na
Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba
kwa mujibu wa sheria za nchi, dawa walizo kamatwanazo wasichana hao
zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na
mtu aliyekamatwa na dawa za kulevya.
AZAM YAZIPA YANGA, SIMBA SHILINGI MIL 280
Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage.
Na Saleh Ally
UONGOZI wa kampuni ya Bakhresa inayomiliki klabu ya Azam umemwaga dola
milioni moja (zaidi ya Sh bilioni 1.6) ili kupata haki ya udhamini wa Ligi Kuu
Bara kama warushaji wa matangazo ya televisheni.
Kutokana na kumwaga fedha hizo, kampuni hiyo
kupitia kituo chake kipya cha televisheni yake ya Azam TV, kitakachoanza kurusha
matangazo hivi karibuni, kitapewa haki ya kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu
Bara.
Kampuni hiyo iliyokuwa inapambana na Supersport
ya Afrika Kusini iliyokuwa tayari kutoa dola 500,000 imeihakikishia bodi ya ligi
hiyo kuwa iko tayari kutoa fedha hizo na kila klabu zikiwemo Yanga na Simba
zitapata Sh milioni 140 kila moja kwa msimu.
CHADEMA YATUPA KOMBORA JIPYA TENA....!!!
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanikiwa kunasa siri za mipango ya hujuma zilizokuwa zimeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne za Jiji la Arusha, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika, zimebainisha kuwa CHADEMA katika uchaguzi huo kilifanikiwa kushinda kata hizo baada ya kuvunja ngome ya CCM iliyok
uwa ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Kwa mujibu wa habari hizo, mipango karibu yote iliyokuwa ikifanywa na CCM, ikiwemo halali na haramu, ilivuja na kufika mikononi mwa wapinzani wao ndani ya muda mfupi hata kabla ya utekelezaji.
Imedaiwa kwamba baadhi ya watu waliokuwa katika kambi ya CCM, waliamua kwa siri kufichua mipango hiyo na kuifikisha kwa mahasimu wao kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa kushiriki katika mambo ya kidhalimu.
Habari zinasema maofisa kadhaa wa CCM ambao wamekuwa wakiratibu na kusimamia mipango karibu yote miovu dhidi ya wapinzani, waliamua kwenda kinyume na makubaliano hayo, na kwa njia ya siri wakafanikiwa kutoa mpango mzima hadharani.
KAULI YA BAN K-MOON JUU YA MAUAJI YA ASKARI WA JWTZ DARFUR
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNO), Ban K-Moon(pichani chini), amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa na mauaji ya askari saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililofanywa na waasi wa Sudan Julai 13, mwaka huu.
Askari hao wa JWTZ waliokuwa Darfur, Sudan ya Kusini kulinda amani kwa mujibu wa UNO, walishambuliwa na waasi hao karibu na kambi ya Manawashi eneo la Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala ambapo pia askari wengine 17 walijeruhiwa baadhi yao vibaya.
Katika salamu zake hizo kupitia kwa Msemaji wake, Katibu Mkuu huyo wa Uno, ameelezea masikitiko yake kuhusiana na vifo hivyo na kutoa pole kwa familia za marehemu waliokuwa wakilinda amani, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani (Unamid).
Ban K-Moon amelaani shambulio hilo dhidi ya Unamid na kuelezea matumaini yake kwamba Serikali ya Sudan itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.
CHADEMA: TENDWA ALIBARIKI KUANZISHWA ‘RED BRIGADE’
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimesema Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alibariki kuundwa kwa makundi ya vijana ndani ya chama hicho, yanayoitwa ‘Red Brigade’.
Hatua hiyo ya Chadema imekuja baada ya Tendwa kutishia kuifuta Chadema, iwapo wataendelea na mpango wao wa kuanzisha kambi za mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchini.
Katika taarifa yake, aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, na kusainiwa na Naibu Msajili, Rajab Juma kwa niaba yake, Tendwa alieleza kushangazwa na kusikitishwa na hatua hiyo ya Chadema kwa kuwa walishakatazwa mpango huo tangu mwaka 2004.
“Msajili anavikumbusha vyama vyote vya siasa hasa Chadema kuwa, kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya siasa kinampa uwezo wa kufuta usajili wa chama chochote kinachokiuka masharti ya usajili au kifungu chochote cha sheria ya vyama vya siasa. Kifungu cha 20 cha sheria ya vyama vya siasa kinasema uamuzi wa msajili ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa rufaa mahakamani,” alisema Msajili.
Subscribe to:
Posts (Atom)