Monday, November 24, 2014
MDAHALO WA JAJI WARIOBA KESHO DAR
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.PICHA|MAKTABA
Taasisi ya
Mwalimu Nyerere (MNF), imeandaa mdahalo maalumu wa Katiba utakaofanyika
kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City ambao mzungumzaji mkuu atakuwa
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alisema
jana kwamba mdahalo huo wa amani ni kwa ajili ya Watanzania wenye
mapenzi mema na utakuwa wa wazi, ikiwa ni sehemu ya kuziba pengo la
mdahalo wa Katiba uliovunjika Novemba 2 ambao ulifanyika kwenye Hoteli
ya Blue Pearl.
Ulivunjika baada ya kutokea vurugu zinazodaiwa
kuanzishwa na kikundi cha watu kwa lengo la kuvuruga uwasilishwaji wa
ujumbe wa Katiba, huku Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Paul Makonda
akitajwa kinara wa vurugu hizo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
BUNDUKI BANDI YAMLETEA MAAFA
Wakili
anayewakilisha familia ya kijana mweusi mwenye umri wa miaka kumi na
mbili aliyepigwa risasi na polisi katika mji wa Cleveland nchini
Marekani, amesema familia yake itafanya uchunguzi wake sambamba na ule
unaofanywa na Polisi kubaini kilichotokea.
Kijana huyo kwa jina
Tamir Rice mwenye umri wa miaka 12 alikuwa amebeba kile kilichoonekana
kuwa bunduki bandia. Polisi wanadai kuwa kijana huyo alikataa kutii amri
alipoambaiwa asalimu amri.Kifaa walichokuwa nacho polisi ndicho kilibaini kuwa bunduki hiyo ilikuwa bandia.
Inaarifiwa kijana huyo alipigwa risasi mara mbili baada ya kuitoa bunduki yake kiunoni mwake lakini hakujaribu hata wakati mmoja kuielekeza kwa poliso wala kujribu kuifyatua.
Wakili wa familia hiyo amesema kuwa ikiwa watapata kuwa haki za kijana huyo zilikiukwa, familia yake itachukua hatua za kisheria dhidi ya polisi.
Mwanasiasa mmoja anapendekeza sheria ambayo itahakikisha kuwa bunduki bandia zinakuwa na rangi unayong'aa zaidi ili ziweze kutambulika haraka. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MFANYAKAZI KATILI MATATANI UGANDA
Polisi
wamebadilisha mashtaka ya mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera
akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kwa
kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji.
Video
hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila babake
mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi
wenegine. Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.
Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.
Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa mashitaka. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
ROGDERS AKUBALI LAWAMA KIPIGO CHA LIVERPOOL
Kocha
wa Liverpool Brendan Rodgers amesema anapokea lawama zote kufuatia
kipigo cha timu yake ya Liverpool ilichokipata kutoka kwa Cyristal
Palace.
Liverpool ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya pili
katika msimamo wa ligi ya England jana ilipata kipigo cha mbwa mwizi cha
mabao 3 -1 kutoka kwa Crystal Palace.Rodger amesema amekubali kwamba ulikuwa ni wakati mgumu na analazimika kufanya juhudi kubwa ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo ndani ya Liverpool.
Amesema wamesikitishwa na kiwango cha timu pamoja na matokeo mabovu na kwamba kama meneja wa ni lazima achukue lawama. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
SHABIKI WA MPIRA AMNG'ATA MWENZIE KENYA
Mwanamume
mmoja mjini Kisumu Magharibi mwa Kenya, alimng'ata sikio jirani yake
baada ya mechi ya soka ya ligi ya uingereza iliyokuwa na matokeo yasiyo
ya kuridhisha kwa mmoja wao.
Mwanamume huyo ambaye ni shabiki sugu
wa klabu ya soka ya Arsenal aliamua kujiondolea hasira ya klabu yake
kushindwa na Manchester United kwa kumng'ata hasimu wake wa Man U sikio
lake Jumamosi usiku.Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa shabiki huyo sugu wa Arsenal hangeweza kustahimili kukejeliwa na jirani yake shabiki wa Man United baada ya klabu yake kushindwa mabao mawili kwa moja
Mwanamume huyo alifungiwa katika chumba kimoja na wakazi wa mtaa wa Railways mjini humo, ambao walitaka kumuua kwa kitendo chake. Inadaiwa hii ni mara ya pili kwa mwanamume huyo kumng'ata mwenziwe sikio kwa sababu za kisoka. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)