Friday, March 27, 2015

GWAJIMA ASAKWA NA POLISI KWA KUMKASHIFU KARDINALI PENGO

GWAJIMA
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kujisalimisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.


Hatua hiyo ya polisi imekuja baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko, ambapo inadaiwa Mchungaji Gwajima alitoa lugha ya kashfa dhidi ya Kardinali Pengo ambaye alipinga tamko lililotolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) la kuipigia kura ya Hapana Katiba Inayopendekezwa.


Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kamishna Suleiman Kova, imemtaka Mchungaji Gwajima kujisalimisha haraka katika Kituo cha Polisi cha Kati kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

JK ATEUA WABUNGE WAPYA

rais-kikwete
RAIS Jakaya Kikwete amewateua Dk. Grace Puja na Innocent Sebba kuwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga, ilisema uteuzi huo unatokana na mamlaka aliyopewa rais na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e).


Alisema ibara hiyo, inampa mamlaka rais ya kuteua wabunge wasiozidi 10 na kwamba uteuzi wa wabunge hao ulianza Machi 20, mwaka huu. Kibanga alisema kuteuliwa kwao kumekamilisha idadi ya wabunge ambao rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kikatiba.


Alisema awali Rais Kikwete aliwateua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Asha Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria), Saada Salum Mkuya (Waziri wa Fedha) na Janeth Mbene (Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara).


Wengine walioteuliwa awali ni Profesa Sospeter Muhongo, Shamsi Vuai Nahodha, Zakhia Meghji na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 27, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KILIMANJARO KINARA WA POMBE YA VIROBA


Mji wa Moshi, Tanzania

 Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe  hasa ya  viroba,  ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.

Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24.

Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa Matumizi ya Pombe kwa vijana  katika mikoa ya  Kilimanjaro, Mwanza, Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza  kwa unywaji wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

LIL WAYNE AMTANGAZA CHRISTINA MILIAN KUWA MPENZI WAKE MPYA

lil-wayne na mpenzi wake christina-milian
BOSI wa kundi la Young Money, Lil Wayne, amemuweka wazi mpenzi wake mpya, Christina Milian, ambaye ni mmoja wa wanachama wa kundi hilo analoliongoza.
Baada ya kuweka wazi habari hiyo, Wayne kupitia mtandao wa Twitter, aliandika, “Samahani kwa kusubiri muda mrefu kujua nini kinaendelea, kwa sasa hakuna tena maswali nikiwa na Christina, huyu ni mpenzi wangu.”
Wayne ni baba wa watoto watano, na sasa yeye, mpenzi wake huyo na mtoto wake wa kwanza, Regina aliyezaa na mama mwingine wanafanya kazi pamoja katika kundi hilo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...