Sunday, May 04, 2014

DIAMOND AIBUKA KIDEDEA KWA KUNYAKUA TUZO SABA (7) ZA KTMA 2014

Msanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz leo May 3, 2014 amedhihirisha kuwa yeye ni msanii mkali kwa kuchukua tuzo saba katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).
Diamond amejinyakulia tuzo:
Msanii Bora wa Kiume,
Video Bora ya Mwaka.
Mtumbuizaji bora wa Muziki wa Kiume.
Wimbo Bora wa Afro Pop.
Wimbo Bora wa Mwaka.
Mtunzi Bora wa mwaka Kizazi Kipya.
Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana.
Hakika Diamond ameonyesha ukali wake, na kuonyesha kuwa yeye ni bora zaidi na anapendwa na watu.  Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

TAZAMA PICHA 40 ZA MATUKIO YALIYOJILI KWENYE TUZO ZA KTMA 2014 USIKU WA KUAMKIA LEO, DIAMOND AVUNJA REKODI

Wanamuziki Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wakifanya vitu vyao stejini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

BOMU LAUA WATU WATATU MOMBASA

Moja kati ya milipuko iliyowahi kutokea Mombasa
Watu watatu wanaripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Mombasa nchini Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa bomu la mkono lilitupwa kwenye basi katika kituo cha mabasi cha Mwembe Tayari ambao hupendwa kutembelewa na watalii na kusababisha vifo hivyo na wengine kujeruhiwa.
Mlipuko mwingine umetokea katika mtaa wa kifahari wa Nyali.
Kamishna mkuu wa polisi Mombasa, Nelson Marwa, amesema watu 6 wamejeruhiwa na kuwa watu waliotekeleza shambulizi hilo walitoroka kwa Pikipiki.
Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio ya mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Alshabaab la nchini Somalia.
Aidha nchi hiyo imekuwa katika tahadhari tangu mwezi Septemba mwaka jana ambapo wanamgambo wa Alshabaab walivamia kituo cha biashara cha Westgate kilichopo mji mkuu wa Nairobi na kuua watu wapatao 67.
Al Shabaab ni kundi ambalo lina uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo limeapa kulipiza kisasi kufuatia Kenya kutuma majeshi yake nchini Somalia mwaka 2011ambayo yameungana na yale ya Umoja wa Afrika AMISOM. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo BBC

WATU 2000 WAFUKIWA KWA UDONGO AFGHANISTAN


Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa wa karibu mita kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 04, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...