Thursday, May 16, 2013

BAADA YA FERGIE NA SCHOLES - DAVID BECKHAM NAE ATANGAZA KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU


Kustaafu ndio habari iliyoshika hatamu nchini Uingereza hiv sasa - wiki moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hiimchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa EnglandDAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga. Beckham, 38, ameisadia Paris Saint-Germain kubeba kombe la  Ligue 1 kwa mara ya kwanza ndani miaka 19 mwishoni mwa wiki hii.
Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huuA.
Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu”
Becks alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid.
Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer. 

CCM YAWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI


   Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana jana Mjini Dodoma imeipongeza serikali kwa hatua inayoendelea kuchukua katika kuchunguza chanzo cha tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea Kanisani Jijini Arusha.
Bomu hilo lilirushwa Mei Tano mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Kanisa la Romani Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olisiti na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE ameeleza kuwa taarifa hiyo ya serikali iliwasilishwa jana katika kikao hicho na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dokta EMMANUEL NCHIMBI .
Kufuatia tukio hilo, Kamati Kuu imelaani na imeitaka serikali kuharakisha uchunguzi pamoja na kuongeza kasi ya uchunguzi wa suala hilo sanjari na kutafuta mzizi wa matukio hayo pamoja na kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa tukio hilo.

AUNT LULU AAMUA KUACHANA NA MASHOGA....!!


MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amepigwa ‘stop’ kutembea na marafiki wanaodaiwa kuwa ni wanaume wenye vitendo vya kike ‘Kuku Watamu’.

Akizungumza na mwandishi  wetu, Aunty Lulu alisema baada ya kuandamwa na maneno juu ukaribu wake na wanaume hao, mama yake mzazi na mpenzi wake wa sasa ambaye hakutaka kumtaja, wamemzuia ‘kumpiga stop’ kumuona na watu hao.
  
“Sasa hivi ndugu zangu ndiyo wamekuwa marafiki zangu, sitembei kabisa na kuku watamu. Siwezi kumuudhi mume wangu mtarajiwa, mama na hata ndugu wengine, nimeamua kuachana nao,” alisema Aunty Lulu ambaye pia ni mtangazaji ‘deiwaka’.

KOCHA WA TAIFA STAR KIM ATAJA TIMU YAKUIKABILI MORROCO

kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen ameongezewa mkataba wa miaka miwili, leo ametaja kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Morocco mwezi ujao kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwakani.


Katika kikosi hicho, kocha huyo Mdenmark amemuorodhesha kipa wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthez’ pamoja na makipa wengine watatu, Juma Kaseja wa Simba SC, Mwadini Ally na Aishi Manula wa Azam.

Upande wa mabeki amewaita Erasto Nyoni, Aggrey Morris wa Azam, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga SC, Shomary Kapombe wa Simba SC na Yahya Mudathir wa Azam.

Kwa viungo, Poulsen amewaita Haroun Chanongo, Mrisho Ngassa wa Simba SC, Simon Msuva, Frank Domayo, Athumani Iddi ‘Chuji’ wa Yanga SC, Salum Abubakar, Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Azam FC na washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC, John Bocco wa Azam FC, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar na Zahor Pazi wa JKT Ruvu.

UKAHABA WALIGUSA BUNGE


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Kundi la Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige aliyeanzisha mjadala.
Spika wa Bunge, Anne Makinda.

BIASHARA ya ukahaba imeligusa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani Jumanne iliyopita takribani dakika nane zilitumika kuijadili inavyoshamiri na namna ya kuitokomeza.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Kundi la Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige, ndiye aliyeanzisha mjadala asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, baada ya kumuuliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuhusu mpango wa serikali kudhibiti ukahaba.

Magige aliuliza kuhusu fikra za serikali juu ya mpango wa kupeleka muswada bungeni, kuhusu uundwaji wa sheria ya kudhibiti ukahaba nchini.
Swali hilo la Magige, lilikwenda sambamba na maelezo kuwa biashara ya ukahaba inavyoshamiri, inazidi kusababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili.
Alisema, biashara hiyo vilevile ni kichocheo cha kushamiri kwa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi, kuongezeka kwa watoto wa mitaani na kukua kwa uhalifu kwa sababu kuna uporaji hufanyika kwa kuwatumia hao wanaojiuza.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alisema serikali inajitahidi kuimaliza biashara ya ukahaba nchini.

Natoa mualiko kwa LEMA kuja UK kusafisha jina lake, nitalipa ghrama za usafiri na makazi.


Ndugu zanguni,
Baada ya kuona kila kukicha tunaendelea kusikia hizi habari zenye kukera kuhusu kesi inayomkabili mbunge wa Arusha God bless Lema.
Mimi kama rafiki wa zamani wa Lema nimeamua kujitolea kumplipia gharama zote ili aje hapa UK kukanusha uzushi huu ambao ni aibu kwa taifa letu kuwa na mbunge ambaye anatafutwa kwa kesi ya aibu ya kubaka.
Mimi kama wananchi wengine sipendi kuona jina la mheshimiwa lina chafuliwa hivyo nimeamua kuwa nitalipa kila kitu kuanzia tiketi ya ndege, ada ya visa na pia gharama za hoteli, chakula na vinywaji kwa kipindi chote mheshimiwa atakapokuwa hapa.
by Chris Lukosi

KAJALA KUIGIZA FILAMU YA MAISHA YAKE HALISI SEGEREA, APONGEZWA NA KUPONDWA.


News is that actress Kajala Masanja anatarajia kucheza katika filamu ambayo itaelezea maisha yake halisi ya kesi yake iliyokuwa ikimkabili. filamu hiyo itaelezea tangu mwazo wa issue hilo, mahakamani, segerea mpaka anatoka baada ya Wema Sepetu kumtolea faini ya sh. millioni 13. Kajala mwenyewe amesema ni kweli na kwasasa story na script ndiyo vinafanyiwa kazi. Hata hivyo wadau wanaweza kuwa na hamu ya kuiona filamu hiyo kama kweli itafanikiwa kuonyesha mazingira halisi ya mahakamani na segerea kama ilivyokuwa kwa mwigizaji huyo kabla ya kuwa uraiani ikichukuliwa kwamba bado ni shida sana kupata location katika taasisi za serikali hasa huko segerea ambako Kajala mwenyewe aliwahi kusema kuna mambo ya kuhuzunisha sana.

 Kwasasa inadaiwa Kajala anafanya filamu ya Princess Sasha chini ya Wema Sepetu huku tayari baadhi ya watu wakisema Kajala ana haraka sana pengine ameburuzwa na watu kuhusu kucheza story ya kesi yake kwakuwa bado mumewe yupo jela hajatoka lakini tayari yeye amepanga yake huku uraiani. Shabiki mmoja amesema " i think Kajala bado hajashauriwa vizuri kwa time hii kucheza maisha yake halisi hata miezi 2 bado kuisha". mashabiki wake wengine wamesema ni poa tu apige kazi " Kajala Nakuaminia Pamoja Sana Kazi Njema" amesema shabiki yake mmoja.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 16.05.2013

DSC 0198 b6684

DSC 0203 33ab2

DSC 0201 6a9fe

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...