Saturday, July 18, 2015

WAZEE WA KIMILA MONDULI WAMUANGUKIA LOWASSA

Wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa Kimaasai (Malaigwanan) kutoka Wilaya ya Monduli wamemuomba waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kubaki na kuendelea kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu ndicho kilichomlea na anakijua.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Monduli kwa niaba ya Malaigwanan, Mzee Joseph Mesopiro kutoka Kata ya Sepeko wilayani humo alisema viongozi wa mila wanakusudia kutuma ujumbe maalumu kwa Lowassa kumshauri asihame CCM kama baadhi ya watu aliowaita wapambe wanavyomshauri.

“Sote Monduli tumesononeka kwa jinsi vikao vya chama vilivyomtendea mbunge wetu. Bado tunampenda kama ambavyo tunakipenda chama chetu. Tunaamini ataendelea kubaki CCM na kupigania ushindi wa chama katika uchaguzi ujao,” alisema Mzee MMesopiro

TUNAWATAKIA EID MUBARAKA WATU WOTE



Leo ni sikukuu kubwa sana duniani... ina maana kubwa sana kwa waislam na watu wote duniani.

Kwakulijua hili Jambo Tz tunachukua nafasi hii kuwatakia sikukuu njema watanzania wote na dunia kwa ujumla.

OBAMA KUTOTEMBELEA KIJIJI CHA BABA YAKE

Barack Obama

#ObamainKenya ndilo neno linalotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya huku rais huyo akitarajiwa kulitembelea taifa hilo.

Hata hivyo wakaazi wa kijiji cha Kogelo ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa hawatalazimika kufanya maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji cha Kogelo.

''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa nairobi pekee'', alisema bwana Godec akizungumza na runinga ya KTN.

Bibiye Obama Sarah Obama alikuwa amejiunga na wakaazi wa Kogelo akimtaka Obama kuwatembelea kulingana na ripoti za kituo cha habari cha Capital fm.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...