Wednesday, April 17, 2013

HISTORIA YA BI. KIDUDE KWA UFUPI

Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Binti Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia leo mchana  huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa.Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. 

Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa nazi na hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102. 

Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....

Mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.

Bi Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni

Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen.

NDOA YA UWOYA NA NDIKU SASA YAFIKA MWISHO RASMI! KISA NI DIAMOND

Mapenzi bwana! Ukiambiwa yanaweza kuua usibishe kabisa, kwani ukiondoa mifano mingine ya kufikirika, kitu ‘live’ ni kwamba mwanasoka raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alianguka na kuzimia, baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mkewe.Ndikumana, alianguka na kuzimia, asubuhi ya Aprili 8, mwaka huu, baada ya kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda, lililoandika habari ya usaliti wa mkewe, Irene Uwoya, aliponaswa hotelini na mwamuziki, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Habari za kuzimia kwa Ndiku, zimewekwa kweupe na Uwoya mwenyewe, aliyesema: “Maskini Ndikumana wangu, baada tu ya kusoma habari ya mimi na Diamond alianguka na kuzimia.”
Kwa tafsiri, Uwoya anamsikitikia mume wake kuanguka na kuzimia, upande wa pili anajuta kumfahamu Diamond, kwani ndiye aliyemsababishia majanga yote.

MIRATHI YA KANUMBA, BADO NI UTATA.

Ngoma inaonekana kuwa bado ni nzito kuhusiana na mirathi ya marehemu Steven Kanumba kwani taarifa zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa, hakuna kitu kilichofanyika mpaka sasa kutokana na mvutano uliokuwepo ndani ya familia.
 

Akizungumza na Risasi Jumatano hivi karibuni, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema yeye aliamua kukaa pembeni na kumuachia baba wa marehemu, mzee Charles Kusekwa afuatilie suala hilo lakini anashangaa mwaka umepita hakuna kilichofanyika.
Akasema, alisikia mzee huyo alituma wawakilishi wake walishughulikie suala hilo lakini wakachemsha kutokana na kukosa viambatanisho muhimu.
 

“Mimi niliamua kusubiri upande wa baba Kanumba wafungue mirathi kwa sababu Kanumba hakuwa na mtoto kusema nina ulazima wa kuharakisha ili apate haki zake, cha ajabu hakuna kilichofanyika mpaka sasa,” alisema mama Kanumba.
 

Akasema, kutokana na kwamba ametoa muda mrefu kwa mzee Kusekwa kushughulikia suala hilo bila mafanikio, ameamua kuingia ‘front’ mwenyewe ili kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.
Credit:Global Pubishers.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUSAMBAA KWA HABARI ZA MISHAHARA YA WALIMU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII



BI KIDUDE AFARIKI DUNIA

.
 
MSANII WA MUZIKI WA TAARABU NCHINI TANZANIA KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR FATUMA BINT BARAKA MAARUFU KAMA BIBI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA LEO HUKO VISIWANI ZANZIBAR.
 
BI. KIDUDE AMEFIKWA NA MATUTI HAYO LEO KUTOKANA NA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU.
 
BI. KIDUDE  AMESHAWAHI KUFANYA KAZI NYINGI IKIWEMO MHONGO WA JANG'OMBE, KIJITI, ALAMINADURA, YA LAITI, AHMADA NA NYINGINE NYINGI.

Mwana Mziki wa Tanzania AY awa Verified on Twitter


Account ya mtandao wa kijamii ya Twitter ya mwanamuziki maarufu Afrika kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya (AY) yatambulika rasmi na kuwa mwanamuziki wa kwanza hapa Bongo account yake kutambulika yaani (Verified Account) .

Twitter ambayo hufanya hivyo kwa kukuwekea alama ya tick ya blue mbele ya jina lako ili kukutambulisha kwa marafiki, ndugu, jamaa, mashabiki wako wanaokufuata [followers] kuwa wewe ni mtumiaji halisi wa account hiyo walifanya hivyo kwenye account ya Ambwene ndani ya masaa kadhaa yaliyopita.

Twitter pia hufanya hivi ili kukutofautisha na watumiaji wengine wanaoweza kutumia jina lako katika mtandao huo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa watu maarufu katika nyanja mbalimbali.
AY amekuwa mmoja kati ya watanzania wachache ambao account zao zimekuwa hivyo akiwemo mcheza kikapu wa Oklahoma City Thunder(OKC) Hasheem Thabeet [@hasheemthedream], Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete [@jmkikwete] Flaviana Matata [@FlavianaMatata] na Waziri January Makamba

VIGOGO WIZARA YA ARDHI KORTINI KWA UBADHIRIFU

Simoni Lazaro (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Gerald Mango.
Watuhumiwa hao wakiwa mahakamani.
Charles Kijuba akikwepa kamera mahakamani.
MAOFISA watatu waandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi leo wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za ufujaji wa pesa za serikali zaidi ya milioni 200. Watuhumiwa hao ni Simon Lazaro ambaye alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Sera, Gerald Mango, Mkuu wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi , na Charles Kijuba, Kaimu Mhasibu Mkuu.
Watuhumiwa hao wamekana mashitaka na mahakama hiyo imesema kuwa dhamana iko wazi

MAGAZETI YA LEO APRILI 17, 2013

.
.

ANGALIA KILICHOJIRI KATIKA BIRTHDAY YA LULU........!!!

MAKAMBA ASHITAKIWA KWA KINANA

WanaCCM wa Ifakara mjini ‘wamemshtaki’ Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuph Makamba kwa Katibu Mkuu wa sasa wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kwa ahadi yake aliyoitoa 2008 ya kuwapatia Sh1 milioni ambayo hajaitimiza. 

Mwenyekiti wa CCM wa tawi la Ifakara mjini, Felista Chakachaka alisema kwamba mwaka 2008, Makamba alipotembelea tawi hilo, aliwaahidi kuwapatia
Sh1 milioni kwa ajili ya kazi za tawi hilo lakini hakuitekeleza.

Hata hivyo, Makamba aliyeko Bumbuli mkoani Tanga, alisema jana: “Sawa, mimi nilitoa ahadi hiyo, sikuitekeleza, sasa aliyepo si ndiyo anatoa...kwani ahadi za Mwalimu Nyerere si Mzee Ali Hassan Mwinyi kazitekeleza, sawa na ahadi za Benjamini Mkapa ambazo Rais Jakaya Kikwete anatekeleza.

“Huyu wa sasa aliyepo madarakani ndiye chama, ile ni ahadi ya chama, ulifikiri Makamba n’toe fedha yangu mfukoni, ile ni ahadi ya chama,” alisema Makamba.

Akijibu hoja hiyo, Kinana alisema kwa kuwa Makamba aliahidi kiasi hicho cha fedha akiwa katibu mkuu, basi yeye atatoa fedha hizo. “Katika kipindi cha wiki mbili fedha hizo zitakuwa zimeingia katika akaunti yenu..nitawapatia kama alivyoahidi alisema Kinana.
Mbali na kutembelea tawi hilo, Kinana alifungua mashina ya wakereketwa matano mjini Ifakara.Kinana yuko ziarani mkoani humo kuangalia maendeleo ya chama hicho tawala.

SOURCE::MWANANCHI:

MILA POTOFU ZACHANGIA KUONGEZEKA KWA MAAMBUKIZO YA UGONJWA MALARIA MKOANI MBEYA

......................................................................

Na Esther Macha, Mbeya
LICHA ya Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya vyandarua hali hiyo bado imekuwa tatizo kutokana jamii zilizo nyingi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuwa na imani potofu kuhusu matumizi ya vyandarua vyenye dawa kuwa hawapati usingizi na wengine kudai ni njia ya uzazi wa mpango.

Hayo yalisemwa jana Bwana afya katika Ofisi ya Wilaya ya Mbarali Bw.Yona Msyani wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili, kuhusiana na elimu ya ugonjwa wa maralia katika viwanja vya hospitali ya Chimala Mission .
 
Alisema kuwa suala la utumiaji wa vyandarua imekuwa changamoto kubwa kwa katuiika utendaji kazi kwa wataalamu wa afya kutokana na wananchi kuwa na imani potofu juu ya matumizi ya vyandarua vyenye dawa.

“Bado tuna changamoto kubwa sana hivyo inatupasa kujipanga na kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa matumizi ya vyandarua “alisema.

Hata hivyo alisema kuwa imani hiyo potofu si kwa Wilaya ya mbarali tu kwani hali hiyo ilijitokeza wakati wa kampani ya ugawaji wa vyandarua hivyo mwaka 2010 kwa nchi nzima.
Bw. Msyani alisema kuwa kama wataalamu wa afya bado wanaendelea kutoa elimu ya afya kwa wananchi jinsi ya kujizuia na ugonjwa wa maralia ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana potofu waliyojenga wananchi.

Akizungumzia kuhusu vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa maralia ,Bwana afya huyo alisema kuwa maralia I ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Tatizo hili lipo kwa kiasi kikubwa kwa watoto , mwaka 2012 mwezi januari mpaka desemba waliugua watoto 1,635 chini ya umri wa miaka mitano ambapo kati ya hao waliofariki ni 100 kwa mwaka jana kutokana na ugonjwa wa maralia.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...