Friday, July 17, 2015

MSAIDIZI WA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA AJIUNGA NA CHADEMA

 Bw. Jumanne Juma Msunga.

MSAIDIZI wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa CCM ni chama cha kudhulumu haki za wanachama wake. 

Akitangaza uamuzi wake huo jana mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za CHADEMA Mkoani Singida, Msunga alisema ameamua kujinga na CHADEMA, huku akidai kuwa CCM haikutenda haki katika mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa nafasi ya Urais.

Alisema CCM haina shukrani kwani imejaa dhuluma kwani katika mchakato huo baadhi ya Wagombea walikatwa bila kujieleza mbele ya kamati husika.

WATU ZAIDI YA 40 WAFA KATIKA MLIPUKO NIGERIA

Wapiganaji wa Boko haram

Wafanyakazi wa uwokoaji Nigeria wanasema katika eno la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Gombe watu arobaini wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea kwenye soko katika eneo hilo.

Mlipuko wa kwanza umetokea nje ya kwenye maegesho nje ya duka la viatu, na kufuatiwa na mlipuko mwingine muda mfupi baadae.

Mmoja ya wafanyakazi wa uokoaji miongoni mwa waliouwa ni wanawake na watoto. Mashuhuda wa tukio hilo amesema hali ni mbaya kwenye mitaa ya Gombe.

WANAJESHI WANNE WANAMAJI WAUAWA MAREKANI

Rais wa Marekani Barack Obama

Mtu mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wanamajiwa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika mji wa Chattanooga, Tennessee.

Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja. Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani. 

Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.

SIMBA KUCHEZA NA AFC LEOPARDS, SIMBA DAY 2015

Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula akiwa Pamoja na Rais wa Simba Sport Club, Evans Aveva, wakati wa uzinduzi wa Simba Day. 

Dima ya Simba Sports Club ya kuendeleza mabadiliko ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo vya mapato.

Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi Simba Week 2015 Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema ‘’Kila mwaka timu yetu ya Simba imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwa ajili ya kufurahi, kuwatambulisha rasmi wachezaji, jezi za timu na kujiandaa kwa msimu mpya, siku hii imekuwa maarufu kama Simba Day.

FIFA KUZIFANYIA MABADILIKO BAADHI YA KANUNI

Makao makuu ya FIFA

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA lina mpango wa kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuzibana nchi zinazowania kuandaa Kombe la Dunia, zisitumie mwanya wa misaada ya kifedha kwa nchi nyingine kama rushwa.

Kipengele kile kinachoziruhusu nchi zinazoshindania nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia kusambaza pesa katika nchi nyingine huenda kikafutwa. 

Aidha FIFA inazitaka nchi zote zinazowania nafasi hiyo kuzingatia haki za binadamu na sheria za kazi wakati wote. Hivi sasa nchi zinazotupiwa jicho ni Urusi inayoandaa kombe la dunia mwaka 2018 na Qatar inayoandaa 2022. 

ura za kuamua nchi gani italiandaa Kombe la Dunia la mwaka 2026 zitapigwa mwaka 2017 huko Kuala Lumpur, Malaysia. Nchi zinazoiwania nafasi hiyo ni Marekani,Canada, Mexico na Colombia.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...