Monday, June 17, 2013
MKASA MZIMA KUHUSU KUPIGWA KWA MBUNGE NASSARI KATIKA KITUO CHA KURA MAKUYUNI
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Arusha aliyejulikana kwa jina la Kalanga na kulazimika kulazwa katika hopitali ya Selian Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi, kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Akizungumza kutoka eneo la tukio, Mratibu wa wanawake wa Chadema Mkoa wa Arusha Sesilia Ndossi alisema “muda wa saa 5 asubuhi tulienda katika kituo cha kupiga kura cha Zaburi, kumsindikiza Mbunge wa Arumeru ambaye katika Uchaguzi huo yeye alikuwa Wakala.
"Lakini tulipofika hapo tulimkuta raia mmoja mwenye asili ya kisomali akiwaita watu na kuwaambia pigia CCM, ndipo Nassari akamuuliza kwanini unapiga kampeni kituoni...
"Huyo Baba alihamaki, akamrukia Nassari wakamchangia na Diwani mmoja aliyeitwa Kalanga, wakamsukuma akaanguka damu ikaanza kumtoka puani...
"Baada ya hapo,tukalazimika kuingilia kati na kuondoka na Nassari akaenda mahali tulipokuwa tunalala akabadili mavazi akaenda kutibiwa Minjingu,
"Hata tulipofika huko waliendelea kutufuata wakaja na gari imejaa vijana wa kimasai wakimtafuta Nassari. Tulivyoona hivyo, tulilazimika kukodi gari ambayo hawaifahamu ndipo tukamwondoa kumpeleka Arusha hospitali ya Selian kwa matibabu zaidi."
Taarifa zaidi kutoka Makuyuni zinasema walipomkosa Nassari walimpiga dereva wake Gadi Palangyo na Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Monduli, Thomas Kilongola, hadi walipokuja kuokolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Makuyuni.
Hadi tunaandika habari hii Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia suala hili baada ya simu yake kuita bila mafanikio.
PICHA ZA MH. FREEMAN MBOWE AWATEMBELEA MAJERUHI NA WAFIWA WA BOMU LILILOLIPUKA SOWETO JIJINI ARUSHA
Mwenyekiti
wa Chadema, Mh freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless
Lema wakiwa katika uwanja wa Soweto, wakati wa zoezi la kuchukua vipimo
mbalimbali chini ya usimamizi wa wataalamu toka Jeshini.
Mhe.Mbowe na Mhe. Lema wakishauriana jambo..
Eneo
la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu
ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai
kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tank hilo
lilishamabuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari la matangazo
lina majeraha mawili katika mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu
chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.
VIONGOZI NA WAZAZI WAASWA KUFICHUA UOVU DHIDI YA WATOTO
(Picha na maktaba)
Na Mwandishi Wetu Steven Kanyeph.Viongozi wa serikali kwa kushilikiana na wazazi wametakiwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika wanapoona watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili unyanyasaji wa kijinsia, ukeketaji na kuozeshwa katika umri mdogo.
Hayo yamesemwa na mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa ambaye ni mkuu wa wilaya ya kishapu bwana; Willson Mkambaku kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya shule ya msingi Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Bwana Mkambaku amewataka viongozi na wazazi washilikiane kwa pamoja kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya unyanyasaji, ubakaji .ulawiti , na kuhakikisha kuwa watoto wanaendelezwa kielimu kushiriki katika maamuzi , ikiwa ni pamoja na kukomesha ajira kwa watoto.
Aidha watoto waameitaka jamii kwa kushirikiana na viongozi kupiga vita imani potofu zenye kuleta madhara kwa watoto kama vile ukeketaji ,ndoa za lazima, uasherati , mauaji ya vikongwe ,albino pamoja na madawa ya kulevya.,
Madhimisho ya siku ya mtoto wa afrika hufanyika kila mwaka tarehe 16 mwezi wa 6 lengo ni kukumbuka mauaji ya kikatili ya mamia ya watoto wa shule yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto afrika ya kusini mwaka 1976 baada ya watoto kufanya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi.
Kauli mbiu ya madhimisho hayo kwa mwaka huu ni KUONDOA MILA ZENYE KULETA MADHARA KWA WATOTO NI JUKUMU LETU SOTE
WABUNGE WA CHADEMA WAGOMA KUINGIA BUNGENI KUFUATIA BOMU LA ARUSHA...IGP ATOA NAMBA YAKE KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA
Wakati
Jeshi la Polisi nchini limesema limepata taarifa za mwonekano wa mtu
aliyetupa bomu katika mkutano wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Arusha,Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe
amesema wabunge wake leo hawataingia bungeni.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mbowe alisema wabunge hao watawasili
Arusha kwa ajili ya kuungana na wananchi pamoja na wanachama kwenye
msiba huo.
Alisisitiza
kwamba kuanzia leo mahema yatawekwa viwanja vya Soweto kwa ajili ya
kuomboleza msiba huo na mara polisi wakimaliza uchunguzi wao na kutoa
majibu juu ya vifo hivyo, marehemu hao watasafirishwa.
Wakati
Mbowe anatoa kauli hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi
akizungumza jana mjini Arusha na waandishi wa habari, alisema taarifa za
awali zinaonesha mlipuko huo ni bomu la kutupwa kwa mkono (grumeti) na
hivi sasa timu ya wataalamu ikiongozwa na Kamishna wa Operesheni
Maalumu wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja inaendelea na uchunguzi wa
tukio hilo.
Naye
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP),
Said Mwema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ameahidi kupambana
na kuhakikisha wahusika wanapatikana.
Subscribe to:
Posts (Atom)