Thursday, November 20, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS NOVEMBA 20, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

OBAMA KUTANGAZA MABADILIKO YA UHAMIAJI

Rais Barack Obama
Ikulu ya Marekani imesema Rais Obama atatumia muda ambao watazamaji wa televisheni nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi kutangaza mabadiliko makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo.
Inatarajiwa kuwa Rais Obama atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba kuzuia wahamiaji wapatao milioni tano kurejeshwa makwao na badala yake wapatiwe vibali vya kufanya kazi nchini humo.
Rais Obama amesema hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa facebook kabla ya hotuba yake.Tangu kuingia madaraka Obama amekuwa akipigania baadhi ya mabadiliko ikiwemo huduma ya utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa bima ya afya. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BINTI AJINASUA NA NDOA YA MWANAMGAMBO

Raia wengi kutoka Ulaya wamejiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria 

Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi amewasili nchini Uturuki baada ya safari iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua mjini Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa Islamic State.
Monique alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye asili ya Uholanzi na Uturuki.
Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS.
Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BIANCHI KUENDELEA NA MATIBABU UFARANSA

 Jules Bianchi dereva wa F1 wa timu ya Marussia aliyepata ajali katika mashindano ya Japanese Grand Prix Oktoba,5, 2014 
 
Dereva wa magari ya langa langa ya Formula 1 Jules Bianchi ametoka katika hali ya kuwa mgonjwa mahututi na sasa anapua bila msaada wa mashine, wamesema wazazi wake katika taarifa yao.
Dereva huyo wa timu ya Marussia mwenye umri wa miaka 25, alijeruhiwa kichwani alipoligonga gari la kuvuta magari katika michuano ya Japanese Grand Prix Oktoba 5,2014.
Dereva huyo raia wa Ufaransa amehamishwa kutoka hospitali ya mjini Yokkaichi nchini Japan na kupelekwa katika hospitali ya Nice nchini Ufaransa kwa uchunguzi zaidi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

FAINALI ZA CAF 2015: TIMU 15 ZAFUZU


Timu ya Algeria wakishangilia ushindi wa timu yao kufuzu kucheza fainali za Caf 2015 nchini Equatorial Guinea 
 
Matumaini ya eneo la Afrika Mashariki kuwa na timu angalau moja katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea mwaka 2015, yameyeyuka baada ya mwakilishi pekee wa eneo hilo timu ya Uganda kucharazwa na Guinea
mabao 2-0 katika mchezo wa kundi E uliofanyika mjini Casablanca, Morocco, Jumatano.


Timu ya Nigeria mabingwa watetezi hawatashiriki fainali za Caf 2015 baada ya kutolewa katika makundi
Uganda iliyokuwa na pointi 7 kama Guinea ilitakiwa kushinda mchezo huo. Ghana inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 11. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MADAI YA RUSHWA QUATAR: NAJIHISI KUONEWA

Sepp Blatter, rais wa FIFA akiitangaza Qatar kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022
Mfichua siri kuhusu tuhuma za rushwa kutolewa na Qatar ili kuiwezesha nchi hiyo kushinda nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 ameiambia BBC kuwa anaishi kwa hofu kutokana na hatua yake hiyo.
Mwaka 2011, Phaedra al-Majid alidai kuwa maafisa wa Qatar walijitolea kuwalipa maafisa watatu wa vyama vya soka barani Afrika kiasi cha dola milioni moja na nusu ili kuiunga mkono Qatar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani.
Baadaye Bi Phaedra al-Majid aliondoa tuhuma hizo, lakini sasa anasema alilazimishwa kubadili kauli yake. Anasema ameingia katika hali ya uendawazimu ya "kujiona anaonewa kila wakati, hofu na vitisho" (na kwamba atajiona mkosaji maisha yake yote.) 
Kamati ya Qatar ya uandaaji wa Fainali za Kombe la Dunia imesema ushahidi wa Phaedra al-Majid ulitiliwa mashaka na timu ya uchunguzi ya FIFA, na kwamba tuhuma zote zilichunguzwa na kutupiliwa mbali. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...