Sakata la Yanga kugomea udhamini wa
Azam Tv limechukua sura mpya baada ya klabu hiyo kutaka kupewa kitita
cha Sh600 milioni ili kukubali kudhaminiwa na Azam. (HM)
Habari za uhakika ambazo Mwananchi
limezipata zinadai kuwa, Yanga wamepata kiburi cha kugomea udhamini wa
Azam baada ya kuwa na ofa mbili mkononi ya Pepsi na ile ya Zuku.
“Pepsi wanatoa kinywaji chao kipya
Pepsi Cola na wametupa ofa ya Sh600 milioni, Azam walifuatwa na kuelezwa
juu ya ofa hiyo wakakataa Pepsi wasiingie kwa vile ni wapinzani wao kwa
Azam Cola,” kilisema chanzo cha habari.
Chanzo hicho kilisema kuwa, Yanga
waliwapa sharti Azam la kuongeza dau kutoka Sh100 milioni na kama
isingewezekana basi waingie mkataba na Kampuni ya Pepsi.