Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge amesema Serikali imekosa ubunifu na
haitaki kupokea ushauri kuhusiana na vyanzo vipya vya mapato ya uchumi kwa mwaka 2013, Mpango wa Maendeleo wa
Taifa kwa mwaka 2014/15 pamoja na utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka
2013/14, Chenge alisema kuongeza ushuru katika bia, soda, juisi na
vinywaji vikali, kumepitwa na wakati.
Wakati Chenge akieleza hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaja vyanzo mbadala vya mapato vinavyofikia Sh6 trilioni. Katika taarifa yake, Chenge alisema mpaka mwisho
wa mwaka wa fedha 2013/14, Bajeti ilikuwa pungufu kwa Sh2 trilioni, huku
Bajeti ya mwaka 2014/15 ikiongezeka kwa asilimia 8.8 (trilioni 1.6),
huku ikiwa na deni la Sh1.3 trilioni ambalo halikuingizwa katika Bajeti
ya mwaka 2014/15.
“Hali hii inaweza kutafsiriwa kuwa Bajeti ya mwaka
2014/15 tayari ina pengo la Sh4.9 trilioni. Yaani Sh2 trilioni ambazo
hazikupatikana mwaka wa fedha 2013/14 na Sh1.6 trilioni ambayo
imeongezeka ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana na deni la Sh1.3
trilioni.
“Kuna umuhimu wa kuharakishwa kuletwa bungeni
sheria ya bajeti itakayofanya kazi sambamba na sheria mpya ya ununuzi
ili kudhibiti matumizi mabaya kwa nia ya kuweka nidhamu katika
utekelezaji wa bajeti ya Serikali,” alisema Chenge. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz