Wanawake
ambao majina yao hayakupatikana, wakazi wa Sinza, Dar es Salaam
wamekumbana na sekeseke la aina yake la ubakaji kisa kikiwa ni uvaaji
wa vimini ambao kwa sasa umeshika kasi kila kona Bongo...
Mwanahabari
wetu mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa manane, alinyetishiwa tukio
la wanawake watatu kuvamiwa na midume na kufanyiwa kitu mbaya baada ya
kuchaniwa vimini vyao maeneo ya Barabara ya Shekilango, Dar kabla ya
kuokolewa na wasamaria wema.
Wasichana hao, wakiwa wamejipodoa vilivyo na kutinga vimini
vilivyoonesha sawia maungo yao nyeti bila ‘makufuli’, walijikuta katika
hali hiyo mbaya baada ya kurushiana maneno na vijana hao wahuni hivyo
wakaonja joto ya jiwe.
Warembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea Manzese, Dar
walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha pikipiki maarufu
kama bodaboda, walipokaribia Makutano ya Barabara ya Shekilango na
Morogoro, Dar.
“Kila
siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo tumewakomesha, serikali
inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali, wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana
hao.
Mwendesha bodaboda mwingine alimwambia mwandishi wetu kuwa
waliwaeleza wasichana hao kuacha tabia ya kutembea nusu utupu kwani ni
hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha maadili ya Watanzania lakini
walijifanya jeuri ndiyo maana wakawaadabisha.
Aliweka wazi kuwa baada ya kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.
“Madereva
wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia wasichana hao na kuanza
kuwachania nguo kwa maelezo kwamba badala ya kuwa nusu utupu, ni vema
wakakaa uchi wa mnyama kabisa.
“Warembo wawili walifanikiwa kutimua mbio licha ya kuchaniwa vimini vyao lakini mmoja aliyekuwa na ‘mdomo mchafu’
“Shukrani
ziwaendee wasamaria wema waliomukoa kwa sababu kwa vyovyote lazima
angebakwa kwani alikuwa ameshachaniwachaniwa nguo na ku... ,” alisema shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Shuhuda huyo aliongeza kuwa binti huyo alifanyiwa kitu mbaya kwa
kushikwa sehemu nyeti kabla ya wale wenzake waliokimbia kurudi wakiwa
kwenye Bajaj na mabaunsa wao kisha kutokomea na mwenzao aliyekuwa
amehenyeshwa vya kutosha na wanaume
hao.
“Wale
wasichana wawili walirudi wakiwa na Bajaj na mabaunsa, wakasaidiwa na
raia wema ndipo wakafanikiwa kumuokoa mwenzao na kutokomea naye
kusikojulikana,” alisema shuhuda huyo.
Credit: GPL