Wingu jeusi
limeanza kutanda kuhusu hatima ya mzozo wa Ziwa Nyasa kutokana na
msimamo wa hivi karibuni wa kiongozi wa Democratic Progressive Party
(DPP), Peter Mutharika ambaye sasa ni Rais mpya wa Malawi.
Hiyo inatokana na msimamo wa Mutharika ambaye ni
Profesa wa Sheria wa kupinga kuendelea kujadiliana na Tanzania kuhusu
nani mwenye haki ya kumiliki ziwa hilo alioutoa wakati alipowatembelea
wananchi wa Chipoko, kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya uchaguzi
mkuu ambao ulimwigiza madarakani.
Pamoja na kwamba mazingira ya msimamo huo yanaweza
kutofautiana na hali halisi ya sasa, tofauti za kisiasa baina yake na
mtangulizi wake, Joyce Banda zinaweza kuongeza msukumo mpya wa kutaka
kutoendelea na mazungumzo ya mpaka wa ziwa hilo.
Akizungumza na wananchi hao, Profesa Mutharika
aliwatoa wasiwasi na kuwataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa
maelezo kuwa ziwa hilo lipo kwenye himaya ya Malawi na kwamba kuendelea
kujadiliana na Tanzania ni kupoteza muda. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz