Kwa
tukio hili, vijana wa mjini wanasema; kimenuka! Hivi karibuni wanawake
watano ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja walinaswa
usiku mnene wakifanya mapenzi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja
kilichopo Mwananyamala jijini Dar.
Watu
hao walinaswa katika oparesheni kabambe iliyoongozwa na Kamanda Mkuu
wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, OCD Wilbroad Mtafungwa pamoja na
Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai.
Katika
zoezi hilo, polisi walivamia kambi kuu inayotajwa kusheheni wanawake
wanaojiuza iliyopo Mwananyamala A ambapo ‘wauza sukari’ hao hutumia
vyumba vyao kufanya ufuska huo.
Polisi hao walipofika kwenye chumba
kimoja kilichopo eneo hilo, walikumbana na upinzani mkubwa wa watu
waliokuwa ndani na baada ya kufanikiwa kuufungua mlango, waliwakuta
wanawake watano na wanaume wawili wakiwa kimahaba.
Mbali
na hao, polisi walifanikiwa kuwanasa wanawake wengine kwenye vyumba
vyao na baadhi mtaani wakijiuza ambapo walipewa kibano cha hali ya juu.
Imeelezwa
kuwa, wanawake hao wamekuwa na tabia ya kujiuza na wakati mwingine
hukubali kufanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja, hali ambayo ni
hatari sana.
Mkazi mmoja wa eneo hilo, Husein Juma alisema: “Kwanza
tunampongeza Kamanda Mtafungwa kwa operesheni hii, wanawake hawa
wamekuwa ni tatizo kwani wamekuwa wakijiuza waziwazi na kutupa ovyo
kondomu.
Naye Inspekta Swai alisema wamekuwa wakipokea malalamiko
kutoka kwa wananchi wa eneo hilo wakaona ni vyema kuyafanyia kazi
ambapo waliwakamata zaidi ya watu 35, wanawake kwa wanaume wanaohusika.
Monday, April 22, 2013
BI KIDUDE UMEKWENDA, UMEACHA MAJANGA YA WASANII WA KIKE BONGO!, WAJUE BAADHI YAO HAPA
Kishindo
cha kuondoka kwako kwenye uso wa dunia tunayoishi kinaweza kuwa kikubwa
ama kidogo au hakuna kabisa kutokana na mazingira au heshima
uliyojijengea katika jamii.
Fatma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude aliaga dunia wiki iliyopita akiwa na zaidi ya miaka 100. Bado jina lake linatamkwa kwenye vinywa vya wengi na linaweza kuendelea kutamkwa kwa miaka mingi zaidi. Bi Kidude, mwanamke shujaa mzaliwa wa Visiwani Zanzibar alileta mapinduzi katika muziki asilia wa mwambao. Aliitangaza Zanzibar, Tanzania na Bara la Afrika sehemu mbalimbali duniani alipokwenda kwa ziara za kimuziki. Inaaminika alifanya kazi hiyo ya muziki, mafunzo ya unyago na biashara ya hina na wanja kwa zaidi ya miaka 90. Katika kipindi chote, Bi Kidude hakushuka kimuziki hadi pale mdomo ulipoanza kuwa mzito kutokana na uzee miaka 10 kabla ya kifo chake Aprili 17, mwaka huu baada ya kuugua maradhi ya kisukari na kongosho kwa muda mrefu.
Pia inaaminika kuwa ndiye msanii mkongwe zaidi aliyekuwa akipanda jukwaani na umri mkubwa ukilinganisha na wengine unaowajua.
Fatma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude aliaga dunia wiki iliyopita akiwa na zaidi ya miaka 100. Bado jina lake linatamkwa kwenye vinywa vya wengi na linaweza kuendelea kutamkwa kwa miaka mingi zaidi. Bi Kidude, mwanamke shujaa mzaliwa wa Visiwani Zanzibar alileta mapinduzi katika muziki asilia wa mwambao. Aliitangaza Zanzibar, Tanzania na Bara la Afrika sehemu mbalimbali duniani alipokwenda kwa ziara za kimuziki. Inaaminika alifanya kazi hiyo ya muziki, mafunzo ya unyago na biashara ya hina na wanja kwa zaidi ya miaka 90. Katika kipindi chote, Bi Kidude hakushuka kimuziki hadi pale mdomo ulipoanza kuwa mzito kutokana na uzee miaka 10 kabla ya kifo chake Aprili 17, mwaka huu baada ya kuugua maradhi ya kisukari na kongosho kwa muda mrefu.
Pia inaaminika kuwa ndiye msanii mkongwe zaidi aliyekuwa akipanda jukwaani na umri mkubwa ukilinganisha na wengine unaowajua.
Mpango wa bunge kuidhinisha Sheria ya ndoa za jinsia moja Ufaransa wazua kizazaa mjini Paris.
Siku
mbili kabla ya bunge la Ufaransa kuidhinisha sheria inayohalalisha ndoa
za jinsia moja kumetokea maandamano ya dakika za mwisho mwisho mjini
Paris.
Watu
wanaopinga sheria hiyo wamekusanyika katika eneo la Montparnasse la mji
mkuu katika juhudi za mwisho za kuizuia sheria hiyo, huku maandamano
mengine ya kundi hasimu pia yaliandaliwa kuiunga mkono sheria hiyo.
Zaidi ya watu 100 wamekamatwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita katika maandamano mengine ya kupinga ndoa za jinsia moja.
Makundi
ya kutetea haki za binadamu pia yameripoti ongezeko la matusi na
mashambulizi ya kimwili dhidi ya jamii ya mashoga na wasagaji nchini
Ufaransa.
Ufaransa
inatarajiwa kuwa nchi ya 14 kuhalalisha ndoa za jinsia moja, kufuatia
kuidhinishwa sheria hiyo nchini New Zealand wiki iliyopita.
Liewig akabidhi majina ya anaowabakiza Simba.
WAKATI
Ligi Kuu Tanzania Bara ikielekea ukingoni, Kocha Mkuu wa Simba,
Patrick Liewig, tayari ametoa mapendekezo ya wachezaji watakaobaki
Msimbazi.
Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo katikati ya msimu huu akichukua mikoba ya Mserbia, Milovan Cirkovic, aliyetimuliwa.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga,
alisema wachezaji wengi waliopendekezwa na Liewig ni vijana.
“Ni
mapema kuzungumzia usajili katika kipindi hiki, lakini kikubwa ni
kwamba kocha tayari amekabidhi orodha ya wachezaji anaowahitaji
watakaoendelea kuichezea Simba katika msimu ujao.
“Wachezaji hao aliowapendekeza wengi wao ni vijana tuliowapandisha msimu huu na wachache wa timu ya wakubwa ambao amepanga kuwaandaa zaidi,” alisema Kamwaga.
“Wachezaji hao aliowapendekeza wengi wao ni vijana tuliowapandisha msimu huu na wachache wa timu ya wakubwa ambao amepanga kuwaandaa zaidi,” alisema Kamwaga.
TAPELI ANAYETUMIA JINA LA WAZIRI LUKUVI AMTAPELI LOWASSA IRINGA
maofisa wa polisi mkoa wa Iringa wakiweka mtego katika nje ya ukumbi wa St Dominic ili kumnasa tapeli huyo anayejiita ni mtoto wa waziri Lukuvi na kutapeli watu |
Tapeli anayetapeli watu maeneo mbali mbali ya Tanzania kupitia jina la waziri Lukuvi akiingizwa ktk gari maalum leo |
Tapeli Jonathan Wiliam Lukuvi feki akitiwa matatani askari kanzu Iringa |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ,askofu Dkt Boaz Sollo na Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa akimsikiliza tapeli huyo akimpa maneno ya kitapeli Lowassa |
Kijana huyo Tapeli akimsomesha waziri Lowassa ukumbini kwa kuahidi kuchangia 100,000 huku akimwomba kumsaidia misaada zaidi |
Hapa akipelekwa katika gari maalum Hapa akiingizwa katika Taxi tayari kwenda polisi |
LADY JAYDEE AWACHANA TENA CLOUDS..... ANADAI KWAMBA MUNGU SI "RUGE" WALA "KUSAGA"
Baada
ya kipindi kirefu cha kuongea kwa mafumbo dhidi ya wamiliki wa Clouds
FM kuwanyonya wanamuziki akianzia na wimbo wake waJoto Hasira,
mwanamuziki Judith Wambura ameendelea kuishambulia redio hiyo na leo
Jumapili ameamua kufunguka kwa kuwachana live wamiliki wa redio hiyo. Hii ni post yake aliyoipost twitter: Lady JayDee @JideJaydee 1h Naamini kabisa kuwa Mungu sio Ruge wala Kusaga. Atanisimamia kwenye hili #Confidence\ |
BABY MADAHA: NTAWACHANGANYA WANAUME KAMA DIAMOND
STAA
wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema
mwaka huu atawachanganya wanaume kama afanyavyo Nasibu Abdul ‘Diamond’
ili kwenda sawa. Akifafanua kauli yake kwa paparazi wa Stori 3, Baby Madaha aliweka bayana kuwa haoni tatizo kunaswa na Mwisho Mwampamba kama ilivyoripotiwa hivi karibuni wakati huohuo anatoka kisela na mkali wa Bongo Fleva, Juma Kassim ‘Nature’. “Watakoma mwaka huu, lazima niwachanganye sana, mbona wao wanatuchanganya sana kama Diamond vile anavyofanya!” alisema Baby. |
Subscribe to:
Posts (Atom)