Tuesday, March 20, 2018

KISA ABDUL NONDO, IGP SIRRO, DCI NA MWANASHERIA MKUU WAITWA MAHAKAMANI

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wito wa kuwaita Mkrugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufika mahakamani kesho Jumatanoo, Machi 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo.

Taarifa za wito huo umetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole ambaye ametoa taarifa hiyo fupi kupitia kwenye ukurasa wake maalum wa Twitter.

Kambole amesema “Wito umetolewa leo (jana Machi 19) Mahakama kuu mbele ya Jaji Samejikwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani 21/03/2018 kujibu kesi ya Abdul Nondo”.

TRUMP APENDEKEZA ADHABU YA KIFO KWA WAUZA UNGA

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali ikiwemo adhabu ya kifo kwa wale watakaobaninika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Hatua amesema ni kwa lengo la kukabiliana na ongezeko kubwa watumiaji ndani ya Marekani.
Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New Hampshire,wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haliridhishwi nalo.
Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

"Mwezi oktoba tulitangaza tatizo hili kama janga la dharula kiafya ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu kipindi kilichopita. Tumelifanyia kazi na bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola billion sita katika bajeti mpya yam waka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya,ambapo tutakuwa tumetenga kiasi kikubwa cha fedha kuwahi kutokea dhidi ya tatizo hili'.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 20, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...