Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (IEBC), Wafula Chebukati amemtangaza Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais.
Chebukati amemtangaza Kenyatta chama Jubilee kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake, Raila Odinga aliyekuwa anawakilisha Muungano wa vyama vya upinzani (NASA), akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote zilizopigwa.
Aidha, watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa 15,073,662 sawa na asilimia 78.91 kati ya milioni 19 waliojiandikisha kupiga kura huku kura zilizoharibika zikiwa 399, 935.
Licha ya mchuano mkali ambao ulionyesha tangu awali Kenyatta akiongoza lakini Raila na wafuasi wake waliamini ameshinda uchaguzi huo huku akitaka tume imtangaze kuwa mshindi wa urais.
Serikali ya Zimbabwe imekataa ombi la
chama cha MDC-T la kuwaruhusu wafungwa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu
wa nchi hiyo ambao utafanyika mwakani 2018.
Taarifa ambayo imetolewa na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Sheria ya Zimbabwe, Virginia Mabiza imeeleza kuwa hawawezi
kuwaruhusu wafungwa kupiga kura kwani sheria za nchi hiyo haziruhusu.
Aisha Mabiza amekishauri chama hicho
cha MDC-T kuwa kama inataka wafungwa waruhusiwe kupige kura basi watume
maombi katika Bunge la nchi hiyo ili lifanye marekebisho ya kisheria
ambayo yatawapa ruhusa wafungwa kupiga kura.
“Ninashauriwa na washauri watu na
uamuzi ambao ninauchukua ni ambao unaruhusiwa na sheria ya nchi, na kama
ni jambo ambalo linakiuka katiba jambo pekee ambalo linahitajika ni
kwenda Bungeni kuomba kubadilisha sheria,” alisema Mabiza.