Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400 sawa na Sh8.91 milioni
kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12 vinavyotumiwa na
kamati hizo na kwa siku 16 ambazo kamati zitakutana, gharama hizo
zitafikia Sh142.56
Wakati kukiwa na malalamiko kwamba Bunge la Maalumu la Katiba linagharimu fedha nyingi za walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia Sh142.56 milioni kukodi vipaza sauti kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad
alithibitisha kukodiwa kwa vipaza sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12
na kwamba kila gharama ya chumba kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani
(Dola moja ni wastani wa Sh1,650).
Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400
sawa na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12
vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16 ambazo kamati zitakutana,
gharama hizo zitafikia Sh142.56. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz