Shirika la Madaktari wasio na
mipaka Medecins Sans Frontiers wametahadharisha kuhusu wizara ya afya
nchini Liberia kuzidiwa nguvu na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika eneo
la Afrika Magharibi.
Mratibu wa mambo ya dharura wa shirika hilo
nchini humo amesema serikali haikutilia maanani vya kutosha madhara
ambgayo yangesababishwa na ugonjwa huo na kwamba mfumo wa afya kwa sasa
upo katika hali ya kushindwa.Nchini Siera Lione, majeshi yameweka vizuizi katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo.
Raia wa Uingereza ambaye ni mfanya biashara katika eneo la Kanema kaskazini mwa nchini hiyo anaeleza madhara wanayopata kutokana vizuizi vya zilivyowekwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment