Marekani imeendeleza
mashambulizi ya anga kaskazini mwa Iraq kwa lengo la kuwasaidia Wakrud
katika mji wa Erbil dhidi ya wapiganaji wa kiislam wa kundi la Jihad.
Wapiganaji wa kundi hilo la Kiislam hivi
karibuni wameendelea kuimarisha ngome yao katika eneo hilo ikiwa ni
pamoja na kuiteka ngome kubwa ya Iraq katika mji wa Mosul. Jeshi la Marekani limesema limefanya
mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Sunni waliokuwa wamejificha katika
milima iliyo eneo la wakimbizi la Yazid.
Hata hivyo Uingereza imesema inaendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Wakurdi ambapo Ofisa wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Alistair Burt anasema nchi hiyo inaweza kusaidia eshi la Wakurdi.
Wakati huo huo vikosi vya majeshi ya Iraq na vyombo vya usalama vimesambaa katika katika maeneo mbalimbali ya mji wa Baghdad huku kukiwa na hali ya wasiwasi kufuatia kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo ya Iraq Nouri al-Maliki inayodaiwa kuwa ni ya utovu wa nidhamu kwa Rais wa nchi hiyo Fuad Masum.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri hiyo amevunja katiba mara mbili,mara ya kwanza ni pale alipojiongezea muda wa kukaa madarakani,wakati alistahili kutangaza kuvunja bunge. Hata hivyo kipindi chake kiliisha august saba alhamisi iliyopopita.
Hata hivyo papa Francis ameelezea gogoro wa Ira kwamba msingi wake mkubwa ni masuala ya tofauti za kidini. Melfu ya watu nchini Iraq wamekuwa wakilazimishwa na wapiganaji wa kiislam ambao wameimarisha ngome ao kaskazini mwa nchi hiyo.Katika ujumbe wake wa jumapili ,papa Francis ametoa wito kwa dunia kukomesha uhalifu huo unaoendelea nchini Iraq. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment