Saturday, July 25, 2015
WEMA SEPETU ALA ‘NGUMI’ ZA USO UBUNGE SINGIDA
Msanii maarufu wa filamu nchini, Wema Abraham Sepetu amepigwa chini katika kura za maoni kugombea ubunge wa viti maalum Singida.
Aysharose Mattembe ndiye ameibuka kidedea akimtupa kwa mbali Madam Wema aliyeshika nafasi ya nne.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
ZLATAN YUKO TAYARI KUKIPIGA MAN UNITED, ILA ANAHOFIA JAMBO MOJA
Mshambuliaji msumbufu na mwenye
majivuno, Zlatan Ibrahimovic maarufu kama ‘Cadabra’ amesema angependa
kuichezea Manchester United siku moja lakini anahofia ‘ngumi’ za kila
siku na kocha Louis Van Gaal.
Akiwajibu waandishi wa habari
kama yuko tayari kujiunga na mashetani hao wekundu, Cadabra alisema
angeweza kuchezea United lakini anahofia ugomvi wa kutoisha baina yake
na Louis Van Gaal.
Zlatan na Van Gaal hawakuwa na
mahusiano mazuri tangu wakiwa Ajax miaka ya 1990’s lakini moto uliwaka
zaidi baada ya Zlatan kumtaja Van Gaal kama ‘pampasi’ katika kitabu
chake.
Wawili hao hawana urafiki na
kwamba hawawezi kuiva chungu kimoja. Hisia zimekuwa ni nyingi miongoni
mwa mashabiki mara baada ya kocha Louis Van Gaal kutangaza kwamba
atafanya usajili wa kushitukiza wa mshambuliaji siku za usoni.
Hata hivyo Cadabra nahodha wa
Sweden anahusishwa na tetesi za kujiunga na AC Milan ya nchini Italia.
Habari zinasema Zlatan amechoshwa na quality ya ligi nchini Ufaransa na
sasa anafikiria kuihama klabu yake ya Paris St. Germain. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
HATIMAYE WAYNE ROONEY AMJIBU VAN GAAL
Wayne
Rooney amesema yuko tayari kuwa mfungaji bora wa Manchester Unites kwa
mara nyingine na amewapa changamoto wenzake ya kuandika Historia msimu
ujao.
Nyota
huyo wa England alicheza namba nyingi msimu uliopita chini ya Louis van
Gaal na ikifika wakati akashushwa mpaka kiungo cha chini.
Kwasasa Rooney anataka kucheza namba anayoipenda yaani namba 9 na amesema yuko tayari kufunga magoli.
“Niko
tayari kubadili akili yangu na kuwa moja ya wafungaji wa magoli,”
Amesema nyota huyo wa zamani wa Everton ambaye msimu uliopita aliifungia
United magoli 12.
“Nataka kucheza nafasi ya mshambuliaji ambapo nadhani ninaweza kufunga, naamini naweza kulitekeleza hilo”
Msimu
wa 2009-10 na 2011-12, Rooney alifunga magoli 34 kwenye mashindano yote
akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati na kama atarudishwa nafasi hiyo
anaweza kufanya vizuri.
Siku
za karibuni, kocha wa Man United, Louis van Gaal alisema anatarajia
kumtumia Rooney kama mshambuliaji wa kati msimu ujao na maneno haya ya
Wayne ni majibu kwa bosi wake. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

Subscribe to:
Posts (Atom)