Monday, April 11, 2016

WATUMISHI HEWA WAMPONZA MAMA ANNA KILANGO MALECELA

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa. Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.

Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza. Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa Abdul Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja.

"Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema Dkt Magufuli.

Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 11, 2016

20160411_075258 20160411_075309 20160411_075332 
Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz

CHINA KUJENGA VIWANJA 60,000 VYA SOKA KWA MIAKA 6...!!!

China inapania kujenga viwanja 60,000 vya Kandanda katika kipindi cha miaka 6 ijayo.
Uwanja wa taifa wa Beijing
Hayo ni baadhi ya mapendekezo katika ruwaza ya kandanda ya China ya 2050 ya kuifanya nchi hiyo iwe kati ya mataifa makuu duniani katika kandanda. Ripoti moja ya serikali imeelezea mipango ya kuimarisha idadi ya wachezaji na watoto wanaosakata dimba kutimia watoto milioni 50.
Viwanja elfu 60 vitakarabatiwa na vingine kujengwa upya. Kulingana na ruwaza hiyo China itakuwa na vilabu vyenye hadhi ya kimataifa kufikia mwaka wa 2050. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
Rais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa angeli furahishwa mno iwapo timu ya taifa ya China ingelifuzu tena kwa kombe la dunia la kandanda na hata kushinda kombe la dunia.
Aidha rais Jinping pia anaitaka kombe la dunia la kandanda liandaliwa nchini mwake. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz

VAN GAL AISIFIA MAN U

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amesema hajuti kuangushwa na Tottenham katika msimu huu wa majira wa 2014, akisema Manchester United ni 'klabu kubwa'. Manchester United wako alama 12 chini ya Spurs baada ya kuchapwa mabao 3-0 katika uwanja wa White Hart Lane siku ya Jumamosi.

'Changamoto zilikuwa kubwa kwangu katika Manchester United na zitazidi kuwa kubwa' alisema Van Gaal , wako nafasi ya tano. ''Naomba radhi kwa Tottenham lakini Manchetser United ni Klabu kubwa'' Ingawaje United wamepata shida nyingi msimu huu ,Van Gaal , ambaye amekuwa akifanya mazungumzo na Spurs kuhusiana na kuwa meneja, anaamini United bado wako mbele kwa klabu za Uingereza.

Hata hivyo alimpuuzilia mbali mwanahabari ambaye alimuuliza iwapo anajutia kuchagua United dhidi ya Spurs. 'Ni jambo la kuudhi kuuliza hivyo,'' meneja huyo mwenye umri wa miaka 64 alisema. Ni rahisi kuuliza, lakini sawa wewe jifurahishe.

Baada ya Van Gaal kutia sahihi mkataba wa miaka mitatu huko Old Trafford, Tottenham imemteuwa meneja wa zamani wa Southampton Mauricio Pochettino. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...