Meneja wa Manchester United, Louis
van Gaal amesema hajuti kuangushwa na Tottenham katika msimu huu wa
majira wa 2014, akisema Manchester United ni 'klabu kubwa'. Manchester United wako alama 12 chini ya Spurs baada ya kuchapwa mabao 3-0 katika uwanja wa White Hart Lane siku ya Jumamosi.
'Changamoto
zilikuwa kubwa kwangu katika Manchester United na zitazidi kuwa kubwa'
alisema Van Gaal , wako nafasi ya tano. ''Naomba radhi kwa Tottenham
lakini Manchetser United ni Klabu kubwa'' Ingawaje United wamepata shida nyingi msimu huu ,Van
Gaal , ambaye amekuwa akifanya mazungumzo na Spurs kuhusiana na kuwa
meneja, anaamini United bado wako mbele kwa klabu za Uingereza.
Hata hivyo alimpuuzilia mbali mwanahabari ambaye alimuuliza iwapo anajutia kuchagua United dhidi ya Spurs. 'Ni
jambo la kuudhi kuuliza hivyo,'' meneja huyo mwenye umri wa miaka 64
alisema. Ni rahisi kuuliza, lakini sawa wewe jifurahishe.
Baada ya
Van Gaal kutia sahihi mkataba wa miaka mitatu huko Old Trafford,
Tottenham imemteuwa meneja wa zamani wa Southampton Mauricio Pochettino. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
No comments:
Post a Comment