Monday, February 18, 2013

TASWIRA YA MKUTANO WA CHADEMA JIJINI ARUSHA LEO


Viongozi wakiwa tayari washawasili
Wananchi wakiwa mkutanoni
Mwenyekiti taifa (CHADEMA) akisalimia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano
mwenyekiti Mkoa wa Tanga,Said Salehe Mbweto akizungumza
Kamanda akizungumza kwa hisia kukemea propaganda za udini za CCM
Kamanda wa mkoa wa Manyara akihutubia
Kamanda Basil Lema akihutubia
M/kiti Mbowe jukwaani tayari,tayari anazungumziwa sera ya CHADEMA,mfumo mpya wa utawala (majimbo)
Mwenyekiti Taifa akisisitiza jambo.

WASTARA KIPENZI CHA SAJUKI AANZA KUONJA UCHUNGU WA NDOA YAKE,MAMA MZAZI WA SAJUKI AMFANYIA HAYA



IKIWA ni takribani siku siku 47 tangu alipofariki staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, kuna madai kuwa tayari visa vimeanza kati ya mkewe Wastara Juma na mama yake mzazi yaani mkwewe, 

Kwa mujibu wa chanzo makini, mama Sajuki amekuwa akidaiwa kumfuatilia Wastara kwa kila anachokifanya hadi kufikia hatua ya kuwaambia watu wamchunguze.
Chanzo hicho kilidai kuwa Wastara na mama Sajuki walifikia hatua ya kurushiana maneno mbele za watu huku ulemavu wa mjane huyo wa Sajuki ukitajwatajwa.
“Unaambiwa wakija watu kumuombea dua Wastara na kumwambia atapata mwanaume mwingine, mama Sajuki anashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio,” kilidai chanzo hicho.
Mama mzazi wa Sajuki.
Kiliendelea kudai kuwa siku moja Wastara alitembelewa na watu kwenye ofisi yake iliyopo ndani ya nyumba anayoishi, Tabata-Bima, Dar ambapo mama Sajuki alidaiwa kuwafuatilia watu hao akitaka kujua mazungumzo waliyokuwa wakifanya na mkwewe huyo.
Kiliendelea kutiririsha madai kuwa siku ya arobaini ya Sajuki, mama Sajuki aliwaka mbele ya kadamnasi akikasirishwa na kitendo cha Wastara kupiga picha akidai huko ni kujitangaza.
HUYU HAPA WASTARA 
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa sakata hilo lilihamishiwa usiku kwani Wastara naye alikuja juu akiomba waweke kikao ili kuweka mambo sawa mbele ya baba Sajuki, mzee Juma Kilowoko.
Baada ya kujazwa habari hizo, dawati la Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wastara ili kusikia upande wake juu ya ishu hiyo ambapo alisema kuwa pamoja na yote, kwa upande wake anamheshimu mama mkwe wake.
MAMA SAJUKI ALIKUWA NA HAYA 
Alipotafutwa mama, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli nilipata uchungu sana wakati wa arobaini kwani mama aliyekuwa akiendesha dua (Mariam Dedesi), alikuwa akisema tumuombee Wastara apate mwanaume mwingine, kama mzazi ni kweli nililia kwa uchungu na kutamka maneno mazito,” alisema mama Sajuki.

SINA KINYONGO JUU YA PENZI LA DIAMOND NA PENNY"...JOKATE


 
BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.
 
 
Akizungumza katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.
Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.

“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,”alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.

Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama

TASWIRA YA MKUTANO WA CUF MOROGORO, PROF LIPUMBA,MAALIM SEIF HAMAD WAPOKEWA KWA MAANDAMANO.


Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia wananchama na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa hadhala uliopewa jina la mchakamchaka mpaka 2015 ambao ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Hamad akihutubia wananchama na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa hadhala wa mchakamchaka mpaka 2015 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
 Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba kushoto,
Katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Hamad na Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi kulia wakifuatilia matukio kabla ya viongozi wakuu wa chama hicho kuhutubia wananchi.
 Wafuasi na wanachama wa Cuf wakiwa wamekunja ngumi juu wakati viongozi wakuu wa chama hicho wakihutumia maelefu ya wakazi wa Morogoro.
 Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akisalimia wananchama na wafuasi wa chama hicho mara baada ya kuwasilia katika ofisi za wilaya za chama hicho mkoani hapa.
 Wananchama na wafuasi wa chama hicho wakiwa katika maamandano kutoka katika ofisi za chama hicho mtaa wa Boma kuelekea uwanja wa shule yamsingi Kiwanja cha Ndege katika mkutano wa hadhala.
 Sehemu ya magari kutoka Dar es Salaam ambayo yamebeba wanancha na wafuasi wa chama hicho yakielekea katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege.
 Wanachama wa Cuf wakiwa katika maandamano huku Mwenyekiti wa Cuf Taifa Profesa Ibrahim Lipumba akiwa katika gari huku akiwapungia wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakati akielekea katika ofisi za wilaya hiyo mtaa wa Boma.

Mmoja wa wasanii akitumbuiza kabla ya viongozi kuhutubia.

ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 HAPA

 


WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI, DK. SHUKURU KAWAMBWA (MB) LEO AMETANGAZA RASMI MATOKEO YA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE, MAARIFA NA QT.

JUMLA YA WATAHINIWA WALIOFAULU KWA MUJIBU WA MATOKEO HAYO NI  23520 KUANZIA DARA LA I HADI LA II  HUKU KATIKA MCHAKATO HUO WASICHANA WALIOFAULU KATIKA MCHAKATO HUO NI 7178 NA WAVULANA NI 16342.AIDHA WAZIRI KAWAMBWA AMESEMA KUWA WALIOFAULU KWA DARAJA LA KWANZA NI 1641, DARAJA LA PILI NI 6495 NA DARAJA LA TATU NI 15426 NA WALIO FELI NI 24903.

SHULE BORA NI PAMOJA NA ST. FRANCIS GIRL YA MBEYA, MARIAN BOYS YA BAGAMOYO, FEZA BOYS DSM, MARIAN GIRLS BAGAMOYO, NA SIMINI NDIZO ZIPO TANO BORA HUKU SHULE NYINGINE NI KANOSA, JUDE, ST. MARY.

KUPATA MATOKEO HAYO BOFYA HAPO CHINI
MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012

SIPO TAYARI KUKUTANA NA LULU MICHAEL KUTOKANA NA UNYAMA ALIOUFANYA KWA KANUMBA"...MAYA


STAA wa filamu za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa tangu Elizabeth Michael ‘Lulu’ atolewe gerezani kwa dhamana, moyo wake unakuwa mzito kukutana naye.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Maya aliweka plain kuwa kila anapofikiria ukaribu aliokuwa nao na marehemu Steven Kanumba, moyo wake unakuwa mzito kumuona Lulu ambaye alikuwa mpenzi wa marehemu.


“Mh! Kukutana na Lulu ni ngumu sana, sijui hata najisikiaje? Moyo unakuwa mzito sana kukutana naye na sijui kwa nini,” alisema Maya.

YULE MAMA ALIYEMLISHA KINYESI MTOTO NA KUMCHOMA NA MOTO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisaha 

Baadhi ya wakazi wa majengo alikokuwa anaishi mtuhumiwa wakimsifu hakimu kwa hukumu aliyotoa kwa mtuhumiwa huyo
Mtoto Aneth kabla ya kukatwa kwa mkono wake wa kushoto
Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha Wilvina Mkandara(24) kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kumtesa hadi kumsababishia ulemavu mtoto wa shemeji yake.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo alisema mshakiwa amehukumiwa kutokana na kifungu cha 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai cha mwaka 1985.
Amesema Mahakama inaweza kumtia hatiani mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa mazingira au ushahidi wa moja kwa moja ambapo alisema mshtakiwa anahukumiwa kutokana na ushahidi wa mazingira kwa sababu mhangwa wa tukio hilo alishindwa kutoa ushahidi wa moja kwa moja.
Ameongeza kuwa mahakama hiyo imeona mshtakiwa anastahili adhabu kutokana na mtuhumiwa huyo kama mzazi kushindwa kujali afya ya mtoto ili hali alikuwa mama mlezi ikiwa ni pamoja na kumpeleka Hospitali kwa wakati ili apatiwe matibabu.
Ndeuruo amesema pia mahakama hiyo haikuridhishwa na na ushahidi wa mtuhumiwa alioutoa mahakamani kuwa majeraha yaliyokutwa mwilini mwa mhanga wa tukio hilo yalitokana na kuugua kwa tetekuwanga jambo ambalo alisema si la kweli.
Amesema kuwa mshtakiwa ametoa maelezo wakati wa utetezi wake yanayopingana na na maelezoya daktari aliyemtibu mgonjwa alipofikishwa hospitali wakati akitoa ushahidi mahakamani hapo.
Hata hivyo kabla ya kutoa hukumu hiyo Hakimu huyo alisema kutokana na ibara ya 16 ya sheria ya African Charter inayotaka Nchi itunge sheria ya kulinda haki za watoto ambapo Tanzania haina sheria hiyo hivyo kusababisha watu kuwanyanyasa watoto.
Hakimu huyo ametoa wito kwa taasisi zinazohusika kutunga sheria hiyo mara moja ili kulinda haki za watoto ambayo itatamka wazi adhabu kwa wale watakaobainika kuwatesa na kuwanyanyasa watoto.
Kwa upande wake mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa ameiiambia mahakama hiyo kumpa adhabu kali mtuhumiwa huyo ili liwe fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia kama hizo ambao hajakamatwa.
Amesema kitendo kilichofanya na mshtakiwa huyo ni kitendo chakinyama ambacho kinatakiwa kulaaniwa vikali hivyo kupitia adhabu atakayopewa mtuhumiwa inaweza kupunguza unyasasaji kama huyo katika jamii.
Aidha mshtakiwa Wilvina alipotakiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu kabla ya kusomewa aliomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa kile alichodai kuwa ni mjamzito, pia hajui mtoto wake aliyemzaa alipo pamoja na mawasiliano na familia yake.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Ndauruo amesema amesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa cha kuomba kupunguziwa adhabu kutokana nakutomwona mtoto wake hali inayoonesha kutomjali mtoto aliyemtendea kosa.
Ameongeza kuwa Mahakama imefuatilia historia ya nyuma ya mtuhumiwa ambayo haioneshi kama anamatukio kama hayo ambayo aliwahi kuyafanya lakini mtuhumiwa anastahili adhabu kali kama upande wa mashtaka ulivyo sahauri na kutokana na mhanga kuwa na ulemavu wa kudumu.
Amesema mahakama inamhukumu kifungo cha maisha kifungo kitakachothibitishwa na mahakama kuu kutokana na mtuhumiwa kuwa na haki ya kukata rufaa kama ameona ameonewa katika kesi hiyo.
 
Mwanamke huyo alipandishwa kizimbani Novemba 16, Mwaka chini ya Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa aliiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth.

Benki ya CRDB yawashukuru wakazi wa Njombe kwa kuiwezesha kupata mafanikio makubwa.

Mkuu wa kituo cha Tumaini, Sister Coletha Ponela (kushoto) akifuatana na mkuu wa wilaya ya Njombe, Sarah Dumba pamoja na maofisa wa benki ya CRDB wakielekea ukumbi wa kituo cha Tumaini.
Meneja wa tawi la CRDB Njombe, Alison Andrew akiongea na watoto wa kituo cha Tumaini.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba akiongea na watoto wa kituo cha Tumaini.
Watoto wa kituo cha Tumaini wakiimba mbele ya mkuu wa wilaya na wageni kutoka benki ya CRDB.
Maafisa wa Benki ya CRDB wakishusha zawadi walizotoa kwa watoto wa kituo cha Tumaini.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba  akikabidhi zawadi.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB, mkuu wa wilaya, watoto na walezi katika picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB katika picha ya pamoja na mlezi wa kituo pamoja na mkuu wa wilaya.
Watoto wakionyesha michezo ya sarakasi.
Mlezi wa kituo sister Coletha akipokea akipokea zawadi ya Tshirt kutoka Benki ya CRDB.
 Baadhi ya wateja wa CRDB Njombe wakiwa katika tafrija na wafanyakazi wa Benki ya CRDB Njombe.
Njombe Jazz Band walikuwepo kuburudisha wageni waalikwa.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB Njombe wakionyesha ujuzi mwingine wa kusakata rhumba.
Afisa Mikopo wa Benki ya CRDB Njombe akitoa somo la mikopo.
Wafanyakazi na wageni waalikwa wakiburudika kwa muziki.
Mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB Njombe Edward Mwalongo, akitoa ushuhuda wake namna gani amenufaika kibiashara kupitia benki ya CRDB.

Baba Mtakatifu aanza wiki ya kufunga na kutoonekana hadharani.


Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.
 Baba mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.
 Baada ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia, Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.

WAKAZI WA MBEYA WAJITOKEZA KWA WINGI KUIPOKEA TIMU YA MBEYA CITY KWA KUPANDA DARAJA KUSHIRIKI LIGI KUU MSIMU UJAO

Baadhi ya mashabiki wa timu yaMbeya City wakicheza na kusubiri timi iingie toka songea
Ni vituko mtindo mmoja jamaa kwa furaha ya timu ya Mbeya City kupanda daraja kushiriki ligi kuu anataka kuvua suruali


Chales Mwakipesile  Dr Samwel Lazaro  na mhandisi wa barabara wakipanga ratiba ya mapokezi

Hivi ndiyo timu ilivyopokelea maeneo ya uyole jijini Mbeya hapa timu ya Mbeya City inapokelewa na mashabiki wake

Watumishi wa jiji la Mbeya wakionyesha furaha yako kwa kucheza kiduku 

Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakiwa makini kufuatilia matukio ya kuipokea Mbeya City

Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga mara baada ya kushuka toka wenye gari yake na ndiye aliyeongozana na timu hiyo toka songea akishangilia kwa furaha ya timu ya Mbeya City kupanda daraja

Nae pia mkurugenzi wa jiji la Mbeya JumaIdi hakuwa nyuma kuonyesha furaha yake kwa timu yake ya Mbeya City

Ni fuaraha na shangwe tu





Bibi huyu akicheza na kusema sasa tumepata timu yetu hii ndiyo timu ya Mbeya sasa du kumbe wabibi wamo nao kwenye michezo

Mashabiki wa Mbeya City

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Idi na mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla wakikumbatiana kwa furaha wakati wa kuipokea timu hiyo katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Idi akiwashukuru wakazi wa jiji la mbeya kujitokeza kwa wingi kuipokea timu yao ya Mbeya City 

Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga akiongea na wapenzi wa timu ya Mbeya City mara baada ya timu hiyo kuwasili katika viwanja vya ukumbi wa mkapa jijini Mbeya


Wakuu wa idara mbalimbali za jiji la Mbeya wakimsikiliza meya wa jiji

Moja wa viongozi wa timu ya Mbeya City Emmanuel Kimbe akiwashukuru mashabiki na wakazi wa mbeya 

Kocha wa timu ya Mbeya City Juma mwambusi akiongea na wapenzi wa Mbeya City



Mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla akiwaasa wachezaji wa timu ya Mbeya City kuwa sasa ni wakati wa timu hii kuleta kombe la ligi kuu hapa mkoani Mbeya maana hi ndiyo timu yetu wakazi wa mkoa huu 



Picha ya pamoja

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...