Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akihutubia mkutano wa hadhara kijiji cha Mingoyo mkoani Lindi Feb 18,
2013 akiwa katika ziara Lindi mjini kukagua na kuimarisha uhai wa chama.
(Picha na Bashir Nkoromo).
Wananchi
wakiwa kwenye mkutano huo.
Na
Anna Nkinda – Maelezo , Lindi
Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa (NEC) Mama Salma
Kikwete amewataka wakazi wa kijiji cha Kitumbikwela na Mingoyo wilayani
Lindi mjini kuchangamkia punguzo la kuingiza umeme katika nyumba zao na
kuepukana na gharama za mafuta ya taa ambazo zinapanda mara kwa mara.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais aliyasema hayo jana wakati akiongea
kwa nyakati tofauti na wananchi hao katika ziara yake ya kichama ya
kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kuwa mjumbe wa NEC kutoka
wilaya ya Lindi mjini.
Alisema
kuwa miaka ya nyuma gharama za kuweka umeme majumbani zilikuwa kubwa na
kufikia shilingi milioni mbili na nusu lakini hivi sasa zimeshuka hadi
shilingi laki nne na arobaini elfu fedha ambazo hata mwananchi wa
kawaida anaweza akajiwekea akiba na kuzipata.
Mama
Kikwete alisema, “Kuweka umeme katika nyumba yako si utajiri kwani
gharama za uwekaji zimepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma jambo la
muhimu ni nyumba iwe imeezekwa vizuri na kuwekwa nyaya za kuingiza umeme
ndani ya nyumba (wire ring).
Hata
kama hauna hela unaweza kuweka akiba yako kidogokidogo kila mwaka pale
unapouza mazao na baada ya miaka michache utakuwa umepata fedha yote,
nawasihi wananchi wenzangu hakikisheni kuwa umeme utakapofika kijijini
mnautumia kwani wenzenu wanatamani kuwa na umeme lakini bado
haujawafikia”.
Aidha
Mama Kikwete pia aliwashimiza wanawake wajitokeze kwa wingi katika
miradi ya kukopa mbuzi lipa mbuzi na kopa ng’ombe lipa ng’ombe kwani
wakipata fedha kidogo pamoja na za waume zao pato la familia
litaongezeka na hivyo kujikwamua kimaendeleo.
Akiwa
katika kijiji cha Mingoyo aliwasihi wazazi kuwalea vijana wao katika
maadili mema na kuwaelekeza pale ambapo wanapokosea kwani utandawazi
unawaharibu vijana wengi na kujikuta wanajiingiza katika matendo
yasiyofaa ikiwa ni pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya na uvutaji wa
bangi.
“Baadhi
ya vijana wanaona fahari kuwa na wapenzi wengi jambo ambalo ni la
hatari kwa kuwa unajiandalia mazingira ya kupata kirahisi maambukizi ya
virusi vya Ukimwi na takwimu zinaonyesha kuwa kwa kila watanzania mia
moja sita wanamaambukizi. Muache tabia hiyo na kufuata vitabu
vitakatifu vya dini vinavyosema kwani ugonjwa huu hauna dawa zaidi ya
dawa za kupunguza makali tu”, alisema Mjumbe huyo wa NEC .
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Mingoyo Jamridi Mandowa alisema kuwa
tangu Serikali ilipotangaza kuanza kwa mradi wa kusambaza umeme
vijijini, kupunguza gharama za ufungaji wa umeme majumbani na kusogeza
muda wa kupokea maombi wananchi wamejitokeza kwa wingi kutuma maombi
lakini kasi ya usambazaji ni ndogo hawaelewi tatizo ni kitu gani.
Naye
Diwani wa Kata ya Msinjahili ambaye ni Meya wa Lindi Mjini Frank Magali
alisema kuwa kata yake inamradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe na kopa
mbuzi lipa mbuzi ambapo kwa upande wa ng’ombe walipata majike nane na
dume mmoja na kuwakopesha wananchi ambao kwa kiasi kikubwa wamenufaika
na mradi huo.
Mama
Kikwete alifanya mikutano ya hadhara na kujibu maswali ya wananchi wa
kata za Msinjahili, Mingoyo na Mitandi na kuwakabidhi kadi wanachama
wapya wa CCM 37, Umoja wa vijana 37, Umoja wa Wanawake 92 na Jumuia ya
Wazazi 73.
No comments:
Post a Comment