Wafuasi wa (Chadema) wilayani Mpanda
jana jioni walilazimika kutafuta vichochoro vya kukimbilia baada ya
polisi kusambaratisha kwa mabomu ya machozi, maandamano ya kumsindikiza
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe baada ya mkutano.
Patashika hiyo ilitokea baada ya mkutano wa Mbowe
kumalizika na wafuasi wake kutaka kumsindikiza hotelini, jambo ambalo
polisi hawakulikubali.
Baada ya wananchi hao kuanza maandamano hayo,
polisi walifyatua mabomu takriban 15 yaliyowafanya wafuasi wote
kutawanyika na kusababisha taharuki miongoni mwa wakazi wa mji huo.
Dakika chache baada ya tukio hilo, umeme ulikatika mji mzima.
Tofauti na maeneo mengine aliyofanya ziara zake
kama Tabora, Sikonge na Igunga ambayo wafuasi walikuwa wakimsindikiza,
polisi wa Mpanda walijipanga ipasavyo tangu mapema kuhakikisha hali hiyo
haitokei. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz