Kauli ya Interpol inakuja huku kukiwa na
mkanganyiko kuhusu kashfa hiyo iliyosambaa wiki iliyopita kupitia vyombo
mbalimbali vya habari vya kimataifa ambayo hata hivyo, Serikali
imekanusha kupitia Ikulu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Wizara ya Maliasili na Utalii huku ubalozi wa China nchini
nao ukitoa tamko la kukanusha taarifa hizo.
Kamishna wa Interpol Tawi la Tanzania, Gustav
Babile alisema jana kuwa raia hao wa China wanatafutwa popote walipo
duniani na hivyo watakapopatikana watakamatwa.
“Tunawatafuta popote duniani kwa usafirishaji wa
meno ya tembo na uharamia wa mazingira, wakipatikana watachukuliwa
hatua,” alisema Kamishna Babile. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Alisema majina na idadi kamili ya Wachina wanaotafutwa ipo na endapo kuna umuhimu wa kutajwa, yatatangazwa.
Mpaka sasa, mtandao wa Interpol umeweka majina ya
raia wawili wa China, Mingzhi Zhang na Deng Jiyun ambao wanasakwa kwa
tuhuma za kusafirisha meno ya tembo.
Wanadiplomasia kutokaguliwa
Wakati ripoti hiyo ilidai meno hayo yalisafirishwa
kwa ndege ya Rais wa China kupitia maofisa wa kidiplomasia wa nchi hiyo
ambao hawakaguliwi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema
maofisa wataendelea kutokaguliwa kwa kuwa Serikali haiwezi kubadili
sheria za kimataifa za maofisa hao kupata kinga ya kutokaguliwa
wanapokuwa kwenye msafara wa Rais.
“Kwa ninavyojua, ukaguzi wa mizigo kwa misafara ya
kidiplomasia unazingatia na kutawaliwa na sheria za kimataifa kwa hiyo
Tanzania haiwezi kubadili tu kama Taifa,” alisema Balozi Sefue.
Hata hivyo, alisema ni vyema kama Wizara ya Mambo
ya Nje ingezungumzia suala hilo la sheria za kutokaguliwa kwa mizigo ya
maofisa wa msafara wa Rais.
“Ni sheria za kimataifa kwa hiyo ipo, mizigo
ambayo inakidhi vigezo vya kimataifa vya kutofanyiwa ukaguzi na ipo
ambayo haina vigezo hivyo,” alisema Sefue.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe na Katibu Mkuu wake, Michael Haule
hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo lakini ofisa mmoja wa wizara
hiyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema: “Kwa kawaida
mizigo ya wanadiplomasia hao hukaguliwa ila wao wenyewe ndiyo
hawakaguliwi, hilo ndilo jambo msilolielewa, ingekuwa wamebeba kitu
kingeonekana tu.”
Alisema sheria za kimataifa haziruhusu maofisa au rais mwenyewe kukaguliwa mwilini lakini mizigo yao hukaguliwa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Sugu alia na Membe
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mbeya Mjini
(Chadema), Joseph Mbilinyi amesema ni lazima Serikali ifanye uchunguzi
wa kutosha na kuwawajibisha watu waliohusika kuichafua nchi na
utoroshaji wa meno ya tembo badala ya kuja na kauli nyepesi kama
alizotoa Waziri Membe kuhusu ripoti hiyo.
Akichangia Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka
2015/16, Mbilinyi maarufu kama Sugu alisema: “Tanzania imepata coverage
(imeandikwa) juzi kwenye vyombo vya kimataifa kutokana na masuala ya
meno ya tembo, ikisema kwamba uchunguzi huo ulifanyika kwa miaka 10
halafu leo Membe anasimama hapa na kusema ni uzushi.
“Wazungu wanaleta uzushi? Mbona wakisema kwamba
Rais wa Tanzania ni kinara wa utawala bora Membe hakai hapa na kusema
ripoti hiyo ni uzushi?”
Alisema alichokitoa Membe ni mawazo yake na
alichotakiwa kufanya ni kuliambia Bunge kufanyike uchunguzi wa kimataifa
kuhusu suala hilo na ikigundulika kwamba ripoti hiyo ilikuwa ni ya
uongo zichukuliwe hatua kwa hao wanaoichafua nchi.
“Taarifa kama ile kuwa kwenye vyombo vikubwa kama
BBC na Aljazeera ni kuchafua nchi yetu na kwa aina hiyo hatuwezi kwenda
mbele, mambo kama haya wananchi wanahitaji washirikishwe kwani
wanaposikia taarifa kama hizi zinawafanya washindwe kuunga mkono mipango
ya maendeleo kama hii tunayojadili hapa,” alisema Sugu.
“Kila siku tunapiga kelele linaibuka jingine,
mnataka muambiwe hizi pembe zimebebwa na nani ndipo mjue kwamba hili
suala limekuwa kubwa na limefika mahala halikubaliki?”
Alisema ripoti hiyo imeeleza kuwa sababu ya yote
hayo ni rushwa na uongozi dhaifu kwamba kuna udhaifu wa kiuongozi na
Mnyika (John, Mbunge wa Ubungo) aliwahi kusema mkang’aka, lakini leo
dunia imesema suala hilo la rushwa na uongozi dhaifu liwe changamoto ili
kufanikisha mambo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment