Sakata la mke kuishi na waume wawili limechukua sura mpya baada ya
kikao cha ndugu wa mume halali, Rogers Halinga kuketi kikao katika
Kijiji cha Ishungu, Kata ya Ruiwa Mbarali, mkoani Mbeya na kumtaka Biton
Mwashilindi kufanya mazungumzo nao kabla hawajafungua madai ya ugoni
mahakamani na kudai fidia.
Kikao hicho kizito kilichofanyika nyumbani kwa baba mzazi wa Rogers,
mzee Jason Halinga (95), Novemba mosi mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu
lukuki nia ilikuwa kumsikiza mke wa Rogers, Juliana (22) ili abainishe
ukweli juu ya mtoto aliyezua utata kuwa ni wa nani baina ya mumewe
(Rogers) na Biton Mwashilindi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mwanamke huyo akijikanganya mara kadhaa katika kikao hicho akidai
mtoto huyo ni wa Rogers, kwani aliondoka baada ya kutokea mabishano na
mumewe akiwa na ujauzito wa miezi minne ndipo alipoanza mahusiano ya
kimapenzi na Biton hadi siku anajifungua mwaka 2012 akiwa mikononi mwa
Biton na aliamua kumwandikisha mtoto katika kadi ya kliniki kuwa baba
yake ni Biton.
Kutokana na kauli hiyo, ndugu wa Rogers walikuja juu na kumtaka
Juliana atamke wazi mtoto ni wa nani ndipo alijibu kuwa mtoto ni wa
Biton Mwashilindi, ambapo alimkabidhi mtoto huyo mwishoni mwa Oktoba kwa
hiari yake na wala hakuporwa kama alivyotoa taarifa polisi.
Kauli hiyo ya Juliana iliwafanya ndugu wa mume kupiga simu kwa mzazi
wa Juliana anayeishi Lwanjilo wilayani Chunya kujua mustakabali wa kauli
ya mtoto wao kwani ilidaiwa kuwa Biton aliwahi kwenda huko
kujitambulisha kuwa yeye anaishi na mtoto wao kwa kuwa hakujua kuwa
Juliana aliwahi kuolewa kwani alidai kuwa yeye ni mwanafunzi wa VETA
Mbeya.
Baba mzazi wa Juliana, Hosea Mwalukasa alipopigiwa simu alidai kuwa
ni kweli Biton alifika kwake lakini hakumpokea kwa kuwa alidai kuwa
Juliana ni mke halali wa Rogers Halinga, akawaambia kuwa kama amezaa na
Juliana amefanya kosa na kwamba atatozwa faini ya ugoni kwani mwanaye
hakuwahi kupewa talaka na Halinga.
Baada ya mvutano wa muda mrefu kikao kiliamua kuwa endapo Biton
anadai kuwa mtoto aliyezaliwa na Juliana aliyefahamika kwa jina la
Zalida Biton (2) ni wake basi alipe fidia ya kuzaa na mke wa mtu kiasi
cha shilingi milioni kumi au n’gombe saba ili aweze kumkomboa mtoto wake
na kwamba Juliana bado ni mke halali wa Rogers.
Rogers Halinga na mkewe wakiwa kwenye kikao.
Kwa upande wake Biton alidai kuwa hayuko tayari kulipa faini hiyo kwa
sababu alikabidhiwa mtoto kihalali na Jeshi la Polisi Oktoba 31, mwaka
huu katika Kituo Kikuu cha Kati mbele ya maafisa wa polisi na kwamba
hana kesi ya kujibu na anasubiri mtoto afikishe umri wa miaka saba ndipo
amchukue.
“Baadhi ya wadau wamelilalamikia Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuamua
masuala ya kisheria katika vituo vya polisi badala ya kufikisha katika
mamlaka za kisheria kama mahakama. Uamuzi uliotolewa umesababisha tatizo
kuwa zito,” alisema ndugu wa Rogers aliyeomba jina lake lisiandikwe
gazetini.
Amedai kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa kipimo cha DNA bado hakijatatua mgogoro huo na kwamba suluhu katika ndoa hiyo ni kitendawili kisicho na majibu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Amedai kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa kipimo cha DNA bado hakijatatua mgogoro huo na kwamba suluhu katika ndoa hiyo ni kitendawili kisicho na majibu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na GPL
No comments:
Post a Comment