Friday, September 11, 2015

MBUNGE WA CCM ATOA 'SALARY SLIP' KWENYE MKUTANO WA ACT


Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), aliyemaliza muda wake, Ally Keissy. PICHA|MAKTABA 

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), aliyemaliza muda wake, Ally Keissy jana aliibuka kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha ACT-Wazalendo na kupinga maelezo kwamba mshahara wake wa ubunge ni zaidi ya Sh10 milioni.

Keissy aliwasili kwenye mkutano huo uliokuwa wa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea mwenza wake, Hamad Yusuph Mussa uliofanyika Kijiji cha Namanyere, akiwa kwenye gari lake aina ya Toyota Land Cruiser. 

Mgombea mwenza, Mussa alipopanda jukwaani, alianza kuhutubia kwa kuwaeleza wananchi kwamba mbunge wao, Keissy anayemaliza muda wake ameshindwa kuwaletea maendeleo, hivyo mwaka huu wasimpe kura zao.

ABUBAKAR ZUBERI ACHAGULIWA KUWA MUFTI MPYA WA TANZANIA


Mufti mpya, Sheikh Abubakari Zuberi (aliyeketi katikati) ambaye amechaguliwa leo na wajumbe wa BAKWATA mkoani Dodoma kuwa Mufti wa Tanzania akichukua nafasi ya hayati Sheikh Issa Bin Simba 

ALIYEKUWA Kaimu Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi amechaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheik Zuberi amewashinda wagombea wengine watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ya juu ya kuwaongoza waislamu katika Mkutano mkuu wa Bakwata ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 550 ambapowajumbe 310 wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) walipiga kura na kumchagua.

Mashehe wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni pamoja na Ally Muhidin Mkoyogole, Khamis Abbas Mtupa na Hassan Ibrahim Kiburwa. 

Mufti Zuberi anakuwa ni Mufti wa tatu kuchaguliwa kushika wadhifa huo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Muftu Issa Shaaban Bin Simba aliyefariki Juni 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Mufti wa kwanza alikuwa Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed. 

Kabla ya kuchaguliwa , Sheikh Abubakar Zuberi alikuwa Naibu Mufiti wa Sheikh Mkuu wa Tanzania na pia Mjumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa nchini.

MAN U YAMRUDIA TENA DE GEA

David De Gea

Manchester United imeanza mazungumzo ya mkataba mpya na mlinda mlango wake David De Gea. 

Mkataba wa sasa na Muhispaniola huyo unafikia ukingoni mwaka 2016 na United wameonyesha matumani ya kurefusha muda wa De Gea kutumika ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi hii ikitokana na mipango ya De Gea kutimkia kunako klabu ya Real Madrid kukwama.

Manager Louis van Gaal hakumtumia mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid mpaka dirisha la usajili lilipofungwa kwa vile hakukuwa na uhakika juu ya mustakabali wake.

Bado haijajulikana kama De Gea ataanza katika mchezo wa jumamosi wa Ligi ligi dhidi ya Liverpool.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...