Monday, November 25, 2013
BALAA TENA SIMBA SC…BASI LAO LA YUTONG LAKAMATWA, KISA MADENI ...!!!
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
BASI kubwa la klabu ya Simba aina ya Yutong, walilopewa na wadhamini wao, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) linashikiliwa na kampuni ya MEM kutokana na deni la zaidi ya Sh. Milioni 40.
Basi hilo lenye thamani ya Sh. Milioni 200 linashikiliwa kwa siku ya pili sasa, linaweza kupigwa mnada baada ya siku 14, iwapo Simba SC itashindwa deni hilo.
Hali hiyo inatokea wakati klabu inakababiliwa na mgogoro mkubwa baina ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Mweyekiti wao, Alhaj Ismail Aden Rage, Mbunge.

Rage hakupokea simu alipopigiwa jioni
hii ili kuzungumzia suala hilo na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius
Mtawala simu yake haikupatikana kabisa.
Jumanne wiki hii Kamati ya Utendaji ya Simba SC ilitangaza kumsimamisha Rage katika kikao chake cha Jumatatu usiku kwa sababu anaendesha klabu kwa kufanya maamuzi yake mwenyewe bila kushirikisha kamati ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (a).
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang'are 'Kinesi' alisema sababu nyingine ni Rage kuahirisha mkutano Mkuu maalum wa katiba ulioidhinishwa na mkutano mkuu bila kuishirikisha kamati.

Subscribe to:
Posts (Atom)