Thursday, April 18, 2013

MAJIRANI WALAMZIMISHA LIONEL MESSI KUNUNUA NYUMBA ZAO BAADA YA KUFULIA

Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi, hivi karibuni alilazimika kununua nyumba za majirani wanaoizunguka nyumba huko Barcelona Hispania bila kupenda.   
Kwa mujibu wa taarifa kutoka SportsGrid ni kwamba majirani wa Messi walikuwa wanazifanyia marekebisho nyumba zao, lakini kwa bahati mbaya wakaishiwa na fedha katikati ya marekebisho hayo huko mjini Castelldefels, Spain, hivyo wakamuomba kijana tajiri Messi azinunue nyumba hizo zilizokuwa kwenye marekebisho na kwa utaratibu Messi akakataa.
Baada ya ombi lao kukataliwa majirani wakaamua kuanza kufanya vitimbi ili Messi aone kero na kuamua kununua nyumba zao, walizikodisha nyumba zao na wapangaji wao wakawa watu wa fujo wenye makelele muda wote na hatimaye vitimbi hivyo vikazidi kuwa kero kwa Baba Thiago na familia yake. Mara ya kwanza Messi alienda kuongea nao waache tabia hizo lakini hali haikubadilika hivyo akaamua kujenga ukuta mrefu wa kuitenganisha nyumba take na majirani - lakini jaribio hilo likawa linaenda kinyume na baadhi ya sheria za Spain kuhusu ujenzi na majirani wakatumia nafasi hiyo kutishia kumshtaki Messi.

Hivyo ili kuepeukana na skendo ya kupelekwa mahakamani Messi akaamua kuwait a wanasheria wake na kuwaambia wafanye taratibu za kisheria kufanya manunuzi ya nyumba zote za majirani waliokuwa wakitaka kuziuza. Hatimaye mpango wa majirani ukafanikiwa na Messi akanunua nyumba zote za majirani wake hivyo kumfanya kuwa mmoja ya watu wanaomiliki maeneo makubwa kwenye sehemu ya Castelldefels, Spain.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...