Monday, December 22, 2014

"WATANZANIA KUNUFAIKA NA AJIRA QATAR" PINDA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Watanzania watanufaika na kipato na maarifa ya teknolojia ya kisasa kutokana na ajira, ambazo watapata katika nchi ya Qatar baada ya mkataba kusainiwa hivi karibuni.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Doha, Qatar wakati akizumgumza na waandishi wa habari ili kuwapa taarifa fupi juu ya mambo yaliyojiri kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwa Sheikh Abdulla, Pinda alisema wamekubaliana kutoa ajira kwa Watanzania kwa sababu nchi hii inahitaji wafanyakazi wengi kwenye sekta mbalimbali na raia wake ni wachache.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 22, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

WAHITIMU 344 WA DARASA LA SABA HAWJUI KUSOMA NA KUANDIKA...!!!

Wanafunzi 344 waliomaliza darasa la saba mwaka huu mkoani hapa wamebainika kuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu. Ofisa elimu wa mkoa, Nestory Mloka alitoa taarifa hiyo juzi katika kikao cha elimu kilichoitishwa kwa ajili ya kuchambua matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuwapangia shule wahitimu waliofaulu.

Mloka alisema kati ya walihitimu hao ambao hawajui kusoma na kuandika, wavulana ni 163 na wasichana 181. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

KIKWETE "HATUWEZI KUENDELEA KWA KUTEGEMEA RAMLI"

Sehemu ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyoko Tengeru, Arusha

Sehemu ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyoko Tengeru Arusha.

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa kamwe Tanzania, kama ilivyo nchi nyingine yoyote duniani, haiwezi kuendelea kwa kutegemea mazingaombwe ama ramli bila kuwekeza kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha, ametaka Watanzania kuacha mwenendo wa kutumia ubishi wa kisiasa kutafuta majawabu ya changamoto za maendeleo akisisitiza kuwa majawabu ya maendeleo yatapatikana katika maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Amewataka Watanzania kuongeza kasi yao ya matumizi ya intaneti akisema kuwa mfumo huo wa habari na mawasiliano ni chimbuko kubwa la elimu ikiwemo elimu ya sayansi kuliko kutegemea kupata elimu hiyo katika magazeti.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MUME AMJERUHI MKEWE KWA SHOKA KISA WIVU WA MAPENZI

Muonekano wa Malaysia.

Mama mwenye watoto watatu anapata matibabu hospitalini nchini Malaysia baada ya mumewe kuvamia mikono yake na miguu nakumcharanga kwa shoka la kucharangia nyama,na baadaye mwanamume huyo kujinyonga .
Mama huyo anatajwa kama K Menaga,amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Kluang upande wa kusini mwa jimbo la Johor baada ya shambulio hilo hatari lililotokea mapema mwezi huu.
Ingawa taarifa kutoka hospitalini hapo zinaarifu kuwa mama huyo ameshatolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya hali yake kuendelea vyema,na amelazwa katika wodi ya wagonjwa wa kawaida.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

WAAMUZI 11 WA KITANZANIA KWENYE ORODHA YA FIFA

Nembo ya shirikisho hilo,iliyo nakshiwa vyema.
 
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa orodha mpya ya waamuzi linaowatambua ,Kwenye orodha hiyo kuna jumla ya waamuzi 18 kutoka Tanzania,miongoni mwa waamuzi hao waamuzi 11 wapya na 7 wa zamani.
Waamuzi wapya wa kati kutoka Tanzania ni Mfaume Ali Nassor kutoka visiwani Zanzibar pamoja na Martin Saanya kutoka Morogoro, pia wamo waamuzi watatu wa kike ambao ni Florentina Zabron ,Jonesia Rukyaa pamoja na Sofia Ismail.
Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wanaume ni Frank John Komba na Soud Idd Lila , kwa upande wa wanawake ni Kudura Omary Maurice,Hellen Joseph Mduma,Dalila Jafari Mtwana na Grace Mawala.
Waamuzi wa zamani wa Tanzania kwenye orodha ya FIFA ,kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni Nkongo na Waziri Sheha Waziri,kwa upande wa waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali,Fernand Chacha,John Longino Kanyenye ,Ali Kinduli na Samuel Hudson Mpenzu .
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

STERLING MWANASOKA BORA CHIPUKIZI

Raheem Sterling.
 
Mshambuliaji kinda wa Liverpool, Raheem Sterling amekabidhiwa Tuzo ya Mwanasoka bora chipukizi mwaka 2014 na Chama cha soka cha England FA.
Sterling alikabidhiwa tuzo hiyo kabla ya Mechi wa ligi kuu ya England kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal wakiwa uwanja wa nyumbani Anfield, ambapo mechi hiyo imemalizika kwa sare ya goli 2-2.
FA imekuwa na utaratibu wa kutoa tuzo ya Mwanasoka bora wa mwaka kwa wachezaji chipukizi wanaofanya vizuri katika mchezo wa soka.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...