Sehemu ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyoko Tengeru Arusha.
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa kamwe Tanzania, kama ilivyo nchi
nyingine yoyote duniani, haiwezi kuendelea kwa kutegemea mazingaombwe
ama ramli bila kuwekeza kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Aidha, ametaka Watanzania kuacha mwenendo wa kutumia ubishi wa
kisiasa kutafuta majawabu ya changamoto za maendeleo akisisitiza kuwa
majawabu ya maendeleo yatapatikana katika maendeleo ya sayansi na
teknolojia.
Amewataka Watanzania kuongeza kasi yao ya matumizi ya intaneti
akisema kuwa mfumo huo wa habari na mawasiliano ni chimbuko kubwa la
elimu ikiwemo elimu ya sayansi kuliko kutegemea kupata elimu hiyo katika
magazeti.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Rais Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza
katika Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson
Mandela iliyoko Tengeru, Arusha, taasisi ambayo hutoa shahada za juu za
uzamili na uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi.
Akizungumza baada ya yeye mwenyewe kuwa ametunukiwa Digrii ya Heshima
ya Uzamivu (PhD Honoris Causa) katika mahafali hayo ya pili, Rais
Kikwete alielekeza sehemu kubwa ya hotuba yake kuelezea umuhimu wa
maendeleo ya sayansi na teknolojia katika uhai na maendeleo ya Tanzania
na taifa lolote duniani.
“Somo tunalolipata ni kwamba hakuna mazingaombwe wala njia ya mkato
ya kujipatia maendeleo ya juu. “Hatuna budi kuwekeza katika kuendeleza
sayansi na teknolojia nchini, kama kweli tunataka kutoka hapa tulipo.
“Hakuna ramli wala pumba za uchawi zinazoweza kuendeleza nchi yetu hata
ukiimwaga pumba hiyo katika kila njia panda ya barabara na sehemu zote
za Tanzania. Bado Tanzania haitabadilika hata inchi moja,” alisema Rais
Kikwete na kuongeza: “Hatuna budi kuwekeza zaidi katika kufundisha
wanasayansi, na katika tafiti na ujenzi wa miundombinu ya kuwawezesha
wanasayansi kufanya tafiti zao. Kwa muda mrefu sana hili ni eneo ambalo
hatukulipa uzito unaostahili.”
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment