Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Watanzania watanufaika na kipato na
maarifa ya teknolojia ya kisasa kutokana na ajira, ambazo watapata
katika nchi ya Qatar baada ya mkataba kusainiwa hivi karibuni.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Doha, Qatar wakati akizumgumza na
waandishi wa habari ili kuwapa taarifa fupi juu ya mambo yaliyojiri
kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Abdulla Nasser Al
Thani.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwa Sheikh Abdulla,
Pinda alisema wamekubaliana kutoa ajira kwa Watanzania kwa sababu nchi
hii inahitaji wafanyakazi wengi kwenye sekta mbalimbali na raia wake ni
wachache.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Hivi sasa wapo Watanzania wanaofanya kazi hapa, lakini ni wachache
mno. Mazungumzo yalishaanza siku za nyuma. Tukisaini mkataba katika muda
mfupi ujao, tutajua ni idadi gani wanahitajika na wanaweza kuja kila
baada ya muda gani,” alifafanua Waziri Mkuu.
“Hapa Qatar kuna uwekezaji mkubwa umefanyika, kwa hiyo wanahitaji
watu wa kufanya kazi kwenye mahoteli, viwandani, na kikubwa hapa
ninachokiona watu wetu watapata kipato, lakini pia watapata ujuzi kwa
maana ya maarifa yanayoendana na teknolojia ya kisasa,” aliongeza.
Akieleza mambo mengine ambayo wamekubaliana kushirikiana kama nchi
rafiki, Waziri Mkuu alisema kuna mambo makuu manne likiwemo hilo la
ajira.
“La kwanza ni kilimo. Hapa Qatar ni jangwa kila mahali. Wamekubali
kuja kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kwa sababu sisi tuko
karibu nao zaidi kuliko Marekani au Brazil,” alisema.
“Wanaweza kupata mchele, matunda, nyama kwa maana ya machinjio na
viwanda vya kusindika nyama, lakini pia katika uvuvi wa samaki. Tunayo
bahari ila mitaji yetu ni midogo. Kwa hiyo wamekubali kuangalia eneo
hilo pia,” alisema.
Alisema eneo la pili ni la gesi na mafuta. “Wamekubali kutusaidia
utaalamu ili tushirikiane nao katika namna ya kutumia gesi kwenye ngazi
ya chini hasa viwanda kwa sababu wenzetu wana uzoefu wa muda mrefu. Hata
kwenye mafuta wameonesha kuwa wako tayari,” alisema.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment