TAARIFA
za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa
kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo
Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10
jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.
Shirima
(47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni
mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha
taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai
kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro,
nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli
hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya
Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.
Inadaiwa
kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea
gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza
maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.
Marehemu
Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia
alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.
Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika
Mfanya
biashara huyu mkazi wa Dar es salaam mzaliwa wa Moshi kilimanjaro
alikutwa na mauti hayo baada ya kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya
hoteli hiyo ambayo alienda kwa lengo la kuuona ukumbi wa tukio hilo
ambao uko gorofa ya tisa ya hoteli hiyo.
Chanzo Cha Mfanyabiashara huyu kujirusha bado hakijafahamika mpaka sasa.
Taratibu za Mazishi ya Marehemu Zinapangwa jijini dar es salaam na tukizipata tutakuhabarisha mapema.
Ndugu Costa shirima ameacha mke na watoto.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mahali Pema Peponi
Amina