KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)
ikiwa chini ya uongozi wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (T)
Limited (PAP), imetangaza kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 20 baada
ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo.
IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme inatarajiwa kushuka zaidi,
kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito. Marekebisho hayo
yaliyotumia zaidi ya Dola za Marekani milioni 25 ( Sh bilioni 42.5),
yamewezesha mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme
wa uhakika kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika Gridi ya Taifa
mara tu baada ya marekebisho yaliyokamilika Desemba mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo,
Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake inaoutoza
kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao sasa utakuwa chini ya bei
ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 ya dola ya Marekani (Sh 391) kwa
kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.