Heka heka katika lango la Hull wakati Arsenal ilipoibuka na ushindi wa 2-0
Mechi kadha zimechezwa kuwania kombe la FA kwa vilabu vya ligi kuu ya England na vile vya madaraja mengine.
Mabingwa
watetezi Arsenal waliweza kuwacharaza Hull City 2-0 ambao wameshindwa
kulipa kisasi baada ya kushindwa katika fainali za mwaka jana timu hizo
zilipokutana. Magoli ya Arsenal yalifungwa na Per Mertesacker pamoja na
Alexis Sanchez.Crystal Palace ilipata ushindi mnono dhidi ya Dover wa mabao 4-0, huku Stoke City ikiicharaza Wrexham magoli 3-1. Sunderland nayo ilivuna goli 1-0 dhidi ya Leeds.
Mechi kumi zimechezwa ambapo kwa ujumla vigogo wa soka England wameonekana kupata matokeo mazuri. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment