Sunday, May 12, 2013

SCHOLES NAE ATANGAZA KUSTAAFU KUICHEZEA MAN UNITED


Wiki hii imeendelea kuwa mbaya kwa mashabiki wa Manchester United, siku chache baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu, leo hii kiungo wa timu hiyo Paul Scholes nae ameamua kumfuata kocha wake kwa kutundika daluga kuitumikia klabu yake pekee katika soka la kulipwa.


Gwiji huyo wa Manchester United mwanzoni alistaafu wakati wa mwisho mwa msimu wa 2010/2011, lakini akaamua kubadili maamuzi na kurejea kwenye timu mwezi January mwaka jana. 
 
 Katika taarifa yake Scholes, 38, alisema:Hatimaye ninatundika daluga zangu kabisa!
"Kucheza soka ndio ilikuwa kila kitu kwangu, na kuwa na na mafanikio kwa muda mrefu kwenye soka ndani ya Manchester United, chini ya meneja bora kabisa wa muda wote, ni heshima kubwa. 

“Timu ipo kwenye hali nzuri na itaendelea kufanikiwa chini ya uongozi wa David Moyes.” 
  Scholes amecheza zaidi ya mechi 700 akiwa na jezi ya United na kesho atakusanya medali yake ya 11 ya kombe la premier league watakapocheza dhidi ya Swansea.

SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WACHOCHEZI WA KIDINI- WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amesema Serikali ina kazi kubwa ya kushughulika na kundi dogo linalojihusisha na lugha za uchochezi wa kidini ambao unachangia kudhoofisha amani ya nchi.


“Tunajua nia yao ni kufanya nchi isitawalike lakini sisi tumesema hatukubali. Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, ulinzi uimarishwe kila mahali, mshingae kuona watu wanawahoji lakini nia njema, ya kurudisha amani yetu,” alisema Waziri Mkuu.


Ametoa kauli hiyo juzi mchana (Ijumaa, Mei 10, 2013) wakati akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya waumini watatu wa Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa mabomu uliotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, mwaka huu kanisani hapo.


Waziri Mkuu amewaomba wanachi kutoka ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kwenye upelelezi wa tukio hilo.

DIAMOND PLATNUM AFANYA JAMBO KUBWA UINGEREZA ,NA KUWA MSANII WA KWANZA BONGO KUUZA WIMBO UINGEREZA

WAKATI baadhi ya wasanii wakijitoa katika mikataba ya kuuza miito ya nyimbo zao kwenye Makampuni ya Simu, Msanii maafuru ndani na nje ya nchi Naseeb Abdul Diamond amekuwa msanii wa kwanza kupata mkataba wa kuuza nyimbo zake kwenye miito ya simu nchini Uingereza.

Diamond ambaye ndiye msanii pekee wa bongo fleva anaelipwa pesa nyingi nchini kutokana na mauzo ya nyimbo zake katika miito ya simu( caller tune), amesema kwamba miito hiyo ya simu itaongeza mauzo ya kazi zake na kwamba watanzania wanaoishi nchini humo pia watapata fulsa ya kusikiliza nyimbo zake kila wakati. 

Mwanamuziki huyo wa Bongo Fleva amepata dili hilo kubwa la kuuza miito hiyo ya simu na kuwa msanii wa kwanza nchini kujipatia kitita kikubwa cha fedha kupitia nyimbo zake(caller tune) Nchini Uingereza. 


Dili hilo limeonyesha kumfurahisha sana Diamond kwani tayari anaamini kuwa kazi anayoifanya ni nzuri na inaweza kusikilizwa na watanzania waishio Uingereza na Waingereza pia kwa kununua miito ya simu wakiwa nnchini humo. 

Msanii huyo anajivunia suala hilo kwa sababu itawezesha watanzania waishio nchini Uingereza kupata nyimbo zake kwa wakati unaotakiwa tofauti na ilivyo sasa. 
Diamond Platinum ambaye hivi karibuni alikumbwa na kashfa ya kudanganya umma kuwa mpenzi wake wa sasa ambaye ni mtangazaji wa Runinga katika kituo cha DTV Peniel Mungilwa 'Penny' ni mjamzito wa miezi mitatu alikuwa nchini humo kwa ziara ya kisanaa. 
Hata hivyo mwana dada huyo alikanusha taarifa hizo na kudai kwamba hana ujauzito wa msanii huyo na kwamba hajawai kubeba ujauzito wake.

YANGA YATENGA MIL 50 KUMUUA MNYAMA MEI 18

yanga 45743
Yanga
YANGA imeweka fungu la Sh.150 milioni mezani kuwapa motisha wachezaji wake iwapo wataifunga Simba Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mgawo huo kila mchezaji atalamba shilingi milioni tano taslimu.

Hiyo ni kama advansi. Uongozi pia umetenga fungu jingine la Sh.100 milioni kwa ajili ya sherehe za Jangwani baada ya mechi ya Simba, kwenda Bungeni, Dodoma pamoja na Zanzibar.

Awali Yanga walikuwa wamewaahidi wachezaji wake zawadi ya Sh.100 milioni lakini jana Ijumaa Ibrahim Akilimali ambaye ni Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga alitamka kwamba wameongeza Sh. 50 milioni na kufanya ziwe Sh.150 milioni kwa timu tu.

Hiyo inamaanisha kwamba katika wachezaji 30 kwenye mgawo huo kila mmoja anakunja shilingi milioni tano na chenji chenji.

Akilimali alisisitiza kuwa fungu hilo litahusisha zawadi ya Sh. 70 milioni ya bingwa wa Bara.

Katika hatua nyingine, Yanga imeondoka jana Ijumaa kwa mafungu matatu kuelekea Pemba, Zanzibar kuweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao Kocha Ernest Brandts amesisitiza kuwa anataka mvua ya mabao.

Fungu la kwanza la wachezaji liliondoka asubuhi, la pili likaondoka jioni na la tatu litaondoka leo Jumamosi alfajiri. Kutoka Dar es Salaam mpaka Pemba kwa ndege ni mwendo usiozidi dakika 45. Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 12.05.2013

DSC 0093 d3ab0

DSC 0095 60758

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...