NAIBU
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema atafanya
ziara katika shule zote za msingi na sekondari ili kuwabaini wanafunzi
wanaotumia simu za mkononi shuleni.
Mulugo alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizindua mpango mkakati wa elimu ya haki za binadamu na kuongeza ataanzia Mkoa wa Dodoma na atakaowabaini atawanyang’anya na kuzichoma moto.
Alisema suala la utandawazi limechangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuharibika na kuwa na nidhamu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuwadharau walimu na wazazi.
Mulugo alisema kitendo cha wanafunzi kwenda na simu shuleni kimesababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili, ambapo pia kimechangiwa na baadhi ya wazazi kujifanya wanawapenda watoto wao: “Hivi sasa limekuwa ni jambo la kawaida kuwakuta wanafunzi wa ngazi zote wakiwa na simu shuleni. Mimi sikubaliani nalo, nimeamua nitafanya

ziara
shule moja baada ya nyingine nikimkagua mwanafunzi mmoja baada ya
mwingine nikianzia na Mkoa wa Dodoma katika kipindi hiki cha Bunge. Ole
wake mwanafunzi nitakayemkuta na simu nitamnyang’anya na kuichoma moto
maana walimu wanawalea sana… halafu na mimi mniimbie ‘tunataka haki
zetu’,” alisema Mulugo.