Mwalimu Sofia Mgaya akiwa amelala na watoto wake wote watano kitandani baada ya kujifungua
...............................................................................
Na Nathan Mtega,Songea
WATOTO
watano waliozaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Ruvuma kwa wakati mmoja kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la
Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma wamefariki
dunia baada ya kuishi hai kwa muda wa masaa kumi.
Akizungumza
kwa njia ya simu mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Ruvuma Dkt Benedict Ngaiza alisema kuwa watoto hao watano ambao
walizaliwa kwa njia ya upasuaji wakiwa na umri wa miezi nane tofauti na
inavyotakiwa umri wa mtoto kuzaliwa kuwa ni miezi tisa.
Alisema
kuwa watoto hao mara baada ya kuzaliwa Mei 24 mwaka huu majira ya saa 4
asubuhi walikuwa wakiendelea vizuri ingawa wote walikuwa na uzito mdogo
huku mwenye uzito mkubwa akiwa na gramu 730 na mwenye uzito mdogo akiwa
na gramu 430 na kitendo cha kuzaliwa kabla ya muda stahili wa mtoto
kuzaliwa kimechangia watoto hao kufariki majira ya saa 3 usiku
hospitalin hapo.
Watoto
hao wamezikwa katika makaburi yaliyopo eneo la Lilambo mjini Songea na
kushuhudiwa zaidi na baadhi ya wanawake huku baadjhi ya wadau wakiwemo
viongozi wa serikali wakijipanga namna ya kuwasaidia watoto hao kwa
sababu mama yao ni mwajiriwa mpya wa wizara ya elimu na mafunzo ya
ufundi stadi katika shule ya sekondari Luhawasi iliyopo mjini Songea.
No comments:
Post a Comment