Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil
(kushoto) akimpokea Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi cha siku tatu kinachofanyika katika
Hoteli ya Paradise jijini Mbeya.
Katika Hotuba yake ya ufunguzi,
Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na
watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi akizungumza na wajumbe wa baraza hilo kabla ya kufungua kikao cha
siku tatu kinaofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya.
Wa pili
kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi. Kushoto ni Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe.
Wa pili kushoto ni Venance
Ntiyalundura, Katibu wa tawi hilo. Katika kikao hicho Ntunguja aliwaomba
watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili
kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo.
Sehemu ya
wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya,
Mariam Ntunguja (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya
kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku tatu unaofanyika katika Hoteli
ya Paradise jijini Mbeya.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.