--
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa
Sudan Mheshimiwa Omar Bashir kufuatia kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa
Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la
Darfur na kumtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na
kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha mbele ya
sheria haraka iwezekanavyo.
Katika mazungumzo yao, Rais Omar Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Rais Bashir amemueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini kuwa waliohusika ni wahalifu na hivyo kuahidi kuwa lazima
watasakwa hadi kukamatwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.