Tuesday, February 18, 2014

TAARIFA YA CCM KUHUSU MAAMUZI YA VIKAO VYAKE, KIKUBWA NI KUHUSU ADHABU YA AKINA LOWASSA NA SUMAYE


IMG_2949
Nape Moses Nnauye Katibuwa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari leo mchana katika makao makuu ya CCM Lumumba  ofisi ndogo ya chama jijini Dar es salaam kuhusu maamuzi ya vikao vya chama vilivyomalizika mjinDaodoma hivi karibuni.
…………………………………………………………………………………..
Kati ya tarehe 13/02/2014  na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama.
Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013.
Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:-
1.    Ndg. Frederick Sumaye
2.    Ndugu Edward Lowasa
3.    Ndugu Bernard Membe
4.    Ndugu Stephen Wassira
5.    Ndugu January Makamba
6.    Ndugu William Ngeleja
Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza adhabu.  Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika.
Kwa ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-
1.    Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

UTAJIRI MKUBWA WA VICKY KAMATA WAANIKWA....!!!

WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele…yelele… Hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata anayetajwa kuwa na utajiri balaa.
http://jambotz8.blogspot.com/Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata.

Vicky amepata mafanikio makubwa ambayo kila mwanamke Tanzania angependa kuyapata. Mwandishi wa habari hii alimchimba kwa kina na kupata utajiri wote alionao kwa sasa.
 
KABLA YA SIASA, KABLA YA BONGO FLEVA
Kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania waliozaliwa katika familia duni.
Katika kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, Vicky amewahi kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva na kutunga nyimbo mbalimbali, wimbo wa Wanawake na Maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika jamii.
“Nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda Morogoro. “Kila kitu kinabadilika kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky mwenye watoto wawili, Revocatus na Glory (jina la baba halikutajwa).
 
MAFANIKIO YAANZA
Mwaka 2006, Vicky alifanikiwa kuajiriwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akiwa ni afisa uhusiano.
Mwaka 2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita.
 
MJENGO WA GHOROFA MBILI
Akiwa mbunge, Mheshimiwa Vicky ameingia kwenye orodha ya wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili Sinza jijini Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne.
Ndani ya ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea ‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia yake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 18, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.


.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...